Uchunguzi wa Washington Post kuhusu mashambulio ya Iran kwenye vituo 228 vya kijeshi vya MarekaniUchunguzi wa Washington Post kuhusu mashambulio ya Iran kwenye vituo 228 vya kijeshi vya Marekani

Mwandishi wa habari mpelelezi wa gazeti la Washington Post amechapishwa maelezo kuhusu mashambulizi ya Iran kwenye taasisi na zana 228 za kijeshi za Marekani katika Ghuba ya Uajemi.

Mwandishi mpelelezi wa gazeti la Washington Post amesema: Iran imeharibu au kutia hasara kubwa kwa uchache katika vituo na vifaa 228 vya kijeshi katika kambi 15 za jeshi la Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Katika kisa kimoja, mlipuko mkubwa ulionekana kwenye kambi ya anga huko Imarati kutokana na shambulizi la Iran.

Wataalamu wamesisitiza kwamba kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya kujibu mapigo ya Iran kinazidi sana kile ambacho serikali ya Marekani imetangaza, na kwamba vita vimeonyesha uwezo wa Iran wa kushambulia kambi za Marekani, jambo ambalo wengi walikuwa wamelipuuza.

Wakati huo huo, Wall Street Journal imeripoti kwamba Wamarekani wametumia takriban dola bilioni 45 zaidi kwa ajili ya kununua mafuta ya petroli na dizeli wakati wa vita vya Iran kuliko walivyofanya katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Vilevile, Shirika la Nishati la Kimataifa limeonya kwamba kukarabati hali iliyosababishwa na mshtuko wa usambazaji wa nishati kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz kutachukua miezi kadhaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *