
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei amesema kupanda hadhi ya Iran ya kuwa taifa kubwa na lenye taathira kunahusiana moja kwa moja na ongezeko la idadi ya watu wake, na kutoa wito wa kuzidishwa juhudi za kukuza utamaduni wa kuzaa watoto.
Katika ujumbe alioutoa kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Idadi ya Watu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amejibu barua ya rambirambi na mkono wa taazia kutoka kwa wanaharakati wa masuala ya idadi ya watu kufuatia kuuawa shahidi babake Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
“Miongoni mwa mafanikio ya thamani ya Vita vya Tatu vya Kujihami Kutakatifu na baraka kubwa ya mwamko wa aina yake ulioonyeshwa na wananchi wa Iran ambao umedhihirika wazi kwa kila mtu, ni kuibuka Iran kama nguvu kubwa na yenye ushawishi,” amesema Ayatullah Mojtaba.
Bila shaka yoyote kuendelea hali hii na kufikia kiwango kinachohitajika zaidi kunahusiana moja kwa moja na suala la idadi ya watu.”
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ameongeza kuwa: Hitaji la ongezeko la idadi ya watu wakati mwingine hutazamwa tu kama njia ya kufidia mapungufu ya sera zilizopita.
Amesema, kwa kufuata kwa bidii sera sahihi kuhusu ongezeko la idadi ya watu, taifa kubwa la Iran litaweza kupata uzoefu mkubwa wa majukumu ya kimkakati katika siku zijazo, na kuchukua hatua kubwa kuelekea kuunda ustaarabu mpya wa Kiislamu wa Iran.”
