Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wameibua hoja mbalimbali kuhusu ucheleweshaji wa ukamilishwaji wa barabara pamoja …Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wameibua hoja mbalimbali kuhusu ucheleweshaji wa ukamilishwaji wa barabara pamoja …

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wameibua hoja mbalimbali kuhusu ucheleweshaji wa ukamilishwaji wa barabara pamoja na ukarabati wa zile zilizoharibika, wakisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kunufaika na miundombinu bora ya usafiri na usafirishaji.

Wakichangia katika kikao cha baraza la madiwani, baadhi ya madiwani akiwemo Abeid Mnyanga wa Kata ya Mkulazi, Rahma Zagawila pamoja na Godfrey Fungameza wa Kata ya Bwakila Juu, wameitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) kutoa maelezo ya kina kuhusu mpango wa ukarabati wa barabara zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.

Madiwani hao walieleza kuwa ubovu wa barabara unaendelea kuwasababishia wananchi usumbufu mkubwa, hususan katika shughuli za usafiri, biashara na upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii, hivyo wakaitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Akijibu hoja hizo kwa niaba ya Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Morogoro, Gemmastellah Issaka amesema baadhi ya shughuli za ukarabati zilisimama kwa muda kutokana na mvua kubwa zilizonyesha, lakini kwa sasa wakandarasi tayari wamerudi katika maeneo yao na wanaendelea na utekelezaji wa miradi husika.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Kibena Kingo, amesema ifikapo mwezi Juni mwaka huu madiwani wote wanatarajiwa kutembelea vijiji mbalimbali kwa ajili ya kujionea maendeleo ya miradi inayotekelezwa pamoja na kufuatilia changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *