Bruno Fernandez atwaa tuzo ya Mchezaji Bora EPLBruno Fernandez atwaa tuzo ya Mchezaji Bora EPL

Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, leo Jumamosi, Mei 23, 2026 ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England (EPL), msimu huu.

Ushindi huo unamfanya Fernandez aibuke kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kuitumikia Man United.

Fernandes ameonyesha kiwango bora msimu huu akiwa na Man United akitoa mchango mkubwa katika kuiwezesha timu hiyo kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Fernandes anayeitumikia pia timu ya taifa ya Ureno, katika msimu huu amehusika na mabao 28 ya Man United katika mechi 37 za Ligi Kuu England, akifunga manane na kupiga pasi 20 za mwisho.

Kwa kupiga pasi 20 za mabao, Fernandes amefikia rekodi iliyowahi kuwekwa na Thierry Henry na Kevin de Bruyne ya kupiga idadi kama hiyo ya pasi za mabao kwa msimu.

Mchezaji huyo anaweza kuvunja rekodi hiyo ikiwa atapiga pasi ya mwisho katika mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Aston Villa.

Hiyo ni tuzo ya pili kwa Fernandez kushinda msimu huu baada ya kutwaa pia tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu ya Chama cha Waandishi wa Mpira wa Miguu England (FWA).

Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa kwanza wa Man United kushinda tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England tangu Nemanja Vidic alipofanya hivyo msimu wa 2010/2011.

Kwa kushinda tuzo hiyo, Fernandes amewapiku nyota saba ambao alikuwa anawania nao.

Wachezaji hao ni David Raya, Gabriel Magalhaeis na Declan Rice wa Arsenal, Erling Haaland na Antoine Semenyo wa Manchester City, Igor Thiago wa Brentford na Morgan Gibbs-White wa Nottingham Forest.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *