Mkuu wa jeshi la Pakistan azungumza kwa kina na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini TehranMkuu wa jeshi la Pakistan azungumza kwa kina na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini Tehran

Asim Munir, Mkuu wa jeshi la Pakistan amefanya mazungumzo ya muda mrefu na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araqchi mjini Tehran, huku jitihada za kidiplomasia zikishika kasi ili kuzuia kushtadi hali ya mgogoro katika Asia Magharibi.

Mkutano wa wawili hao ulifanyika Ijumaa jioni na kuendelea hadi usiku. Pande mbili zimebadilishana mawazo kuhusu juhudi na mipango ya kidiplomasia inayoendelea kufanywa ili kuzuia  na kuhitimisha vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, pamoja na njia za kuimarisha amani, utulivu na usalama katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Jeshi la Pakistan limeeleza  katika taarifa yake fupi siku ya Ijumaa kwamba Munir aliwasili Tehran kwa ajili ya mashauriano na kubadilishana mawazo na maafisa wakuu wa Iran.

Katika ziara yake mjini Tehran, Asim Munir na ujumbe aliofutana nao walilakiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Eskandar Momeni. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Mohsin Naqvi pia alihudhuria hafla hiyo ya ukaribisho.

Hii ni katika hali ambayo, Jeshi la Pakistan pia lilmeitaja ziara ya Mkuu wa jeshi la nchi hiyo mjini Tehran kuwa sehemu ya juhudi zinazoendelea za upatanishi.

Marekani na Israel zilianzisha vita vya uchokozi dhidi ya Iran tarehe 28 Februari kwa mashambulizi ya anga ambayo yaliwaua shahidi maafisa wa ngazi ya juu na makamanda wakuu wa Iran na kulenga miundombinu ya kiraia, maeneo ya makazi, taasisi za elimu na maeneo ya kihistoria na kiutamaduni.

Vikosi vya ulinzi vya vya Iran pia vilitekeleza mawimbi 100 ya mashambulizi athirifu dhidi ya malengo nyeti na ya kimkakati ya Marekani na Israel katika eneo zima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *