Mapitio ya mkataba muhimu wa nyuklia yavunjika bila makubaliano, yakiongeza hofu ya kasi ya kuenea kwa silaha za silahaMapitio ya mkataba muhimu wa nyuklia yavunjika bila makubaliano, yakiongeza hofu ya kasi ya kuenea kwa silaha za silaha

Ni baada ya saa tatu usiku siku ya Ijumaa ndipo Balozi Do Hung Viet, Rais wa mkutano huo, na Izumi Nakamitsu, Mkuu wa Idara ya Umoja wa Mataifa ya Upokonyaji na Kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia walianza kuzungumza na wanahabari kutoa maoni yao kuhusu kushindwa kwa Mataifa Wanachama kukubaliana juu ya hatua za kuhuisha NPT, ambao licha ya kuonekana kama nguzo kuu ya juhudi za kimataifa za upokonyaji silaha za nyuklia, sasa una zaidi ya miaka 50 tangu kupitishwa kwake.

Licha ya kuchoka viongozi wa mkutano waeleza kilichojiri

Wakiwa dhahiri wamechoka na njaa kwa kuwa mlo wa mchana ulikuwa ni mkate tu, baada ya juhudi zake zisizozaa matunda za kujaribu kupitisha rasimu ya nne ya hati ya mwisho, Balozi Viet bado alitoa majibu marefu kwa waandishi wa habari waliobaki kumsikiliza yeye na Bi. Nakamitsu.

Balozi Viet alisifu “ushiriki wa dhati na wenye maana” wa wajumbe wa mkutano, lakini alikiri kusikitishwa na kushindwa kwao kupata muafaka na kutumia fursa ya kuufanya ulimwengu kuwa mahali salama zaidi.

Sasa ni miaka 16 tangu ahadi zilizowekwa wakati wa kupitishwa kwa Mkataba mwaka 1970 zirejeshwe au kuimarishwa katika Mkutano wa Mapitio, na mkutano unaofuata hautafanyika hadi mwaka 2031.

Wakati huo huo, wasiwasi kuhusu kasi ya kumiliki silaha za nyuklia unaendelea kuongezeka, huku maghala ya silaha yakiboreshwa na idadi ya silaha ikiongezeka. “Mazingaombwe ya kimataifa ya sasa, ambayo yanatawaliwa na mvutano mkubwa na hatari iliyoongezeka inayosababishwa na silaha za nyuklia, yanahitaji hatua za haraka sana,” alionya Balozi Viet.

“Matokeo ya maana yangekuwa yameuimarisha Mkataba na kuendeleza malengo yake,” alisema, “lakini kwa kukosekana kwa matokeo kama hayo, nina wasiwasi kuhusu mustakabali wa afya ya Mkataba.”

Mataifa yawe makini – Nakamitsu

Bi. Nakamitsu alisema kwamba Mataifa wanachama wa Mkataba yanapaswa kuchukulia kwa uzito mkubwa kushindwa mara tatu mfululizo iwapo yanataka kulinda mfumo huo.

“Uzuiaji uenezaji na upokonyaji silaha ni pande mbili za sarafu moja,” alisema akiwahimiza mataifa yenye silaha za nyuklia. “Ni makosa kudhani kwamba wajibu wa kuzuia uenezaji utatekelezwa bila wao wenyewe kujitolea na kutekeleza wajibu wa upokonyaji silaha.”

Guterres asikitishwa na mazungumzo kugonga mwamba

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza masikitiko yake juu ya kushindwa kwa mkutano huo kufikia mwafaka, katika taarifa iliyotolewa Ijumaa.

Pamoja na kupongeza ushiriki wa dhati na wa maana wa mataifa wanachama, alisikitika kwamba mkutano huo haukufanikiwa, hasa katika kipindi hiki chenye changamoto kubwa zinazotishia usalama wa kimataifa.

Bwana Guterres ametoa wito kwa mataifa yote kutumia kikamilifu njia zote zilizopo za mazungumzo, diplomasia na majadiliano ili kupunguza mvutano, kupunguza hatari za nyuklia na hatimaye kuondoa tishio la nyuklia.

Kupata kwa kina kilichojiri bofya hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *