
Zoezi la upigaji kura kwenye baadhi ya maeneo ya Oromia na Amhara nchini Ethipia, liliahirishwa kutokana na hofu za kiusalama, hata hivyo misururu mirefu ya wapiga kura ilionekana kwenye miji mingine, tume ya uchaguzi nchini humo ilisema.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kabla ya uchaguzi huo kuanza hapo jana, kulikuwa na hofu kwamba baadhi ya maeneo yangekosa kushiriki uchaguzi kutokana na suala la usalama.
Kando na Oromia na Amhara, Jimbo lote ka Tigray kaskazini mwa Ethiopia halikushiriki kwenye uchaguzi huo, licha ya utulivu kuanza kurejea baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa amani wa mwaka 2022.
Takwimu za tume ya uchaguzi zinaonyesha zaidi ya vituo Elfu 50 vya kupiga kura vilifunguliwa, wakati 143 vikifungwa kutokana na hofu ya usalama.
Waziri Mkuu Abiy Ahmed, ambaye aliingia madarakani mwaka wa 2018, amesifu hatua ambazo nchi yake imepiga tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1991.
Waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika wakiongozwa na Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta, wamewaambia wanahabari kwamba uchaguzi huo ulikuwa ukiendelea vizuri.