Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni ya “Tunakuona Mbali” yenye lengo la kuwawezesha Watanzania kufikia malengo yao ya maendeleo kupitia huduma rasmi za kifedha, huku ikichochea ujumuishaji wa kifedha na ukuaji wa uchumi jumuishi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NBC, David Raymond, alisema kampeni hiyo inalenga kuwasaidia wananchi kujenga utamaduni wa kuweka akiba, kuwekeza, kupata mikopo na kutumia huduma za kifedha kwa ufanisi ili kutimiza ndoto zao za maisha na biashara.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *