Tathmini hiyo iliyotolewa hivi karibuni na nani?????? imebainisha kuwa kati ya mwezi Aprili na Agosti mwaka huu, zaidi ya watu milioni 2, karibu mmoja kati ya watatu nchini humo wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhakika mdogo wa chakula (daraja la 3 la IPC au zaidi), ikiwa ni pamoja na watu 262,000 walio katika hali ya Dharura (Daraja la 4 la IPC). 

Hali hiyo inaonesha uafadhali kidogo ukilinganisha na makadirio ya awali ya kipindi cha Aprili hadi Agosti mwaka 2026 katika uchambuzi uliochapishwa mwezi Novemba mwaka 2025, ambao ulitabiri watu milioni 2.29 kuwa katika Awamu ya 3 ya IPC au zaidi. 

Hii inatokana na mwenendo mzuri wa mvua na uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo, pamoja na utoaji wa msaada wa kibinadamu wa chakula ambao haukutarajiwa katika uchambuzi uliopita.

Migogoro ya silaha yachangia ukosefu wa chakula

Pamoja na hayo, hali hiyo kwa mujibu wa tathimini ya IPC bado inatia wasiwasi na inaonesha kuzorota kutoka kipindi cha mwezi Septemba mwaka 2025 hadi Machi mwaka 2026 ambapo watu milioni 1.92 walikabiliwa na hali mbaya zaidi (Daraja la 3 au zaidi). Uchambuzi umeeleza kuwa,“Migogoro ya silaha inayoendelea, kutawanyika kwa watu, bei kubwa ya chakula na mafuta, uwezo mdogo wa kaya kufanya manunuzi, na ubovu wa barabara vinaendelea kuzuia upatikanaji wa chakula katika sehemu kubwa ya nchi.

Wakati huu ambao mpango wa msaada wa kibinadamu kwa ajili ya kukabili uhakika mdogo wa chakula unatarajiwa kuwafikia watu 91,000 katika wilaya tisa za nchi hiyo, msaada huo bado hautoshelezi kwa kiasi kikubwa, ukiwafikia asilimia 17 tu ya watu walio katika Awamu ya 3 au zaidi huku ufadhili wa mwaka 2026 unafikia takriban asilimia 10 tu ya mahitaji ya kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *