
Watu 12 wameuawa na wengine 9 kujeruhiwa katika ufyatuaji risasi katika makazi yasiyo rasmi katika kitongoji cha Cleveland jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa mauaji hayo yamejiri jana usiku na kwamba washambuliaji “walisogea katika eneo hilo hilo la makazi, wakaanza kuwafyatulia risasi wakazi wa kitongoji hicho kabla ya kutoroka eneo la tukio kwakutumia gari moja.
Kwa mujibu wa eNews Channel Africa; polisi walifika eneo la tukio majira ya sasa kumi na moja jioni kwa saaa za Afrika Kusini na kukuta waathirika wengi wakiwa na majeraha ya risasi. Wanaume wanane na wanawake watatu wamethibitishwa kupoteza maisha katika tukio hilo la ufyatuajiri risasi huku mwanaume mmoja akifariki dunia baadaye baada ya kufikishwa hospitalini.
Mamlaka husika jijini Johannesburg pia zimeeleza kuwa washukiwa zaidi ya 10 waliokuwa wamejizatiti kwa silaha nzito wanaodaiwa kusafiri kwa kutumia gari nyeupe aina ya Toyota Quantum walifyatua risasi katika maeneo kadhaa ya kitongoji hicho cha makazi ya watu kabla ya kukimbia.
Makazi yasiyo rasmi nchini Afrika Kusini ni maeneo ya makazi ambayo hayajapangwa ambayo kawaida hujengwa kwa muundo wa mabanda.
HIvi karibuni kumeshuhudiwa matukio kadhaa ya uffyatuaji risasi nchini Afrika Kusini katika mawili ya mwezi Disemba waka jana watu zaidi ya 20 waliuawa.
Matukio ya ufyatuaji risasi wakati mwingine yanahusishwa na magenge haramu ya uchimbaji madini ambayo yanaendesha shughuli zao ndani na karibu na Johannesburg. Cleveland ni kitongoji kinachodaiwa kufanyika shughuli haramu za uchimbaji madini.