• Mwanamke mmoja wa Kenya sasa amefichua kitendo kinachodaiwa kuwa cha ajabu cha mfanyakazi wake wa nyumbani aliyekimbia kupitia picha za CCTV zilizoenea mtandaoni
  • Mfanyakazi huyo wa nyumbani anaripotiwa kuwa alifanya vitendo visivyofaa na kumuacha mwajiri wake akihesabu hasara kubwa kabla ya kutoweka akiwa na mkoba uliojaa vitu
  • Mwajiri huyo sasa anaomba msaada wa umma kumtafuta mfanyakazi huyo aliyepotea ili kurejesha mali zilizoibwa

Mwanamke mmoja wa Kenya ameshiriki video kadhaa za CCTV kwenye mitandao ya kijamii huku akimtuhumu mfanyakazi wake wa nyumbani aliyekimbia, ambaye anadaiwa kufanya vitendo visivyofaa kabla ya kutoweka.

Mjakazi
Mwanamke Mkenya sasa anatafuta aliko mfanyakazi wake wa nyumbani. Picha: @Ruthy/TikTok
Source: Facebook

Mwanamke huyo alidai kuwa mfanyakazi wake wa nyumbani, aliyetambulika kwa jina la Ruth, aliiba pesa na nguo zake kisha akatoroka, akimuacha akihesabu hasara.

Katika video zilizowekwa TikTok, mfanyakazi huyo wa nyumbani alionekana akiingia sebuleni na kuchukua pesa kutoka mezani ambazo zinaaminika kuwa za mwajiri wake.

Picha nyingine za CCTV zilimuonyesha akiondoka nyumbani akiwa na begi lililojaa nguo, ambazo mwajiri wake anadai zilikuwa zake.

Pia soma

Aliyenusurika ajali ya Salama akumbuka maneno ya mwisho aliyotamka rafiki yake kabla ya kufariki

Anadaiwa kuvaa nguo hizo zilizoibwa ili kutengeneza baadhi ya video za TikTok kwenye akaunti yake.

“Anaweza kusema kwamba hakuiba chochote, ilhali aliacha nguo zake zote hapa. Aliondoka akiwa na mkoba mkubwa uliojaa nguo zilizoibwa. Alipokuja hapa kwa mara ya kwanza alikuwa na mkoba mmoja tu, lakini kama mnavyoona, aliondoka nao ukiwa umejaa, pamoja na mabegi mengine. Wizi wa aina hii ni mbaya sana. Yeyote anayejua alipo tafadhali awasiliane nami,” aliandika katika maelezo ya video hizo.

Mwajiri huyo tangu wakati huo ametoa video zaidi akisema kwamba anataka kujua alipo mfanyakazi huyo wa nyumbani ili aweze kurejesha vitu vilivyopotea.

Baadhi ya video hizo zilionyesha kile mfanyakazi huyo wa nyumbani alikuwa akifanya wakati mwajiri wake hayupo nyumbani. Shughuli zake nyingi zilikuwa kulala kwenye kochi, kutazama video na kufanya mazoezi ya kile kilichoonekana kuwa dansi za TikTok.

Tazama baadhi ya video hapa chini:

Mfanyakazi wa nyumbani wa Nairobi amkashifu mwajiri wake

Katika habari nyingine, mwanamke mmoja wa Nairobi ambaye alikuwa akifanya kazi kama mfanyakazi wa nyumbani hivi karibuni alifunguka kuhusu fedheha aliyohisi baada ya kugundua kuwa mwajiri wake alikuwa akimfuatilia kwa siri kupitia kamera za CCTV za nyumbani.

Pia soma

Dereva wa trela amnyima lifti ajuza katika barabara kuu ya Mombasa–Nairobi usiku

Kulingana na mfanyakazi huyo wa zamani wa nyumbani, aligundua kuhusu kurekodiwa huko baada ya kuwa tayari ameacha kazi.

Alidai kwamba mwajiri wake baadaye alimtumia kipande cha video kilichorekodiwa na mfumo wa CCTV.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *