
Ufaransa itawekeza euro milioni 655 zaidi katika maendeleo ya Akili Bandia ili “mapinduzi haya yawanufaishe raia wa Ufaransa,” ametangaza Waziri Mkuu wa Ufaransa, Sébastien Lecornu, siku ya Jumanne, usiku wa kuamkia ufunguzi wa maonyesho ya biashara ya VivaTech huko Paris, kuhusu teknolojia mpya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Programu ya uwekezaji wa umma kwa uvumbuzi, Ufaransa 2030, “itatenga euro milioni 655 zaidi kwa maendeleo ya akili bandia,” Waziri Mkuu amesema katika video iliyorushwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Uwekezaji huu “utasaidia miundombinu, uwezo wa mahesabu, utafiti, biashara, na sekta za viwanda,” alielezea. Waziri Mkuu alisema anatumai “mapinduzi haya yatawanufaisha raia wa Ufaransa,” “kulinda uhuru wetu,” na “kuimarisha huduma zetu za umma.”
Hata hivyo, Sébastien Lecornu alitangaza kwamba kitengo cha idara ya ujasusi wa ndani (DGSI) kimeamua kusitisha mkataba wake na kampuni kubwa ya uchanganuzi wa data ya Marekani Palantir, ambayo mwanzilishi wake mwenza Peter Thiel yuko karibu na Donald Trump. DGSI hatimaye “ilichagua” kampuni ya Ufaransa ChapsVision. “Hatuwezi kukubali utegemezi mpya wa kimkakati katika ulimwengu wa kidijitali,” alielezea. Lengo: “kujenga uhuru wa kweli” ili “tusitegemee nia njema ya baadhi ya washirika, wenye uwezo (…) wa kukata ufikiaji” wa Akili Bandia (AI).