Katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha wafanyakazi na wastaafu wanaishi maisha mazuri wakati na baada ya kumaliza ajira zao taasisi ya Core Securities Ltd imezindua mfuko binafsi wa uwekezaji ambao ni maalum kwa wastaafu na wastaafu watarajiwa kutokana na changamoto kubwa iliyopo inayowakumba wastaafu wengi ambao wanakosa njia sahihi ya kuwekeza.

Uzinduzi wa Foresight Private Reteriment Fund(FPRF), au wekeza kustaafu umezinduliwa rasmi hii leo na mtaalamu wa masuala ya Soko la Mitaji Tanzania Ibrahim Mwangalaba ambapo mfuko huo ambao ni wa kwanza wa Binafsi nchini unatarajiwa kuwa neema kwa wastaafu na wastaafu watarajiwa kutokana na urahisi wa uwekezaji wake ambapo kwa sasa mstaafu anaweza kununua kipande kwa Thamani ya shilingi 100 ya kitanzania ambapo kwa kuanzia mstaafu anaweza kuanza kuwekeza kwa vipande 1000.

Kwa upande wa Taasisi ya Core securities Ltd, kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wake CPA George Fumbuka ameeleza lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo binafsi na malengo ambako kwa kuanzia wanatarajiwa kuanza na kuuza kwa vipande vyenye thamani ya shilingi Bilioni 10, Huku kwa upande wa wadau wa mifuko ya uwekezaji nchini Chama cha waalimu wameweka wazi umuhimu wa kuanza kuwekeza katika mfuko huo ambao ni nafuu kwa wanachama wao.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *