#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limekemea vikali vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kuwataka Watanzania kuwathamini na kuwalinda watoto wenye mahitaji maalum ili wapate haki zao za msingi.

Kauli hiyo imetolewa wilayani Kibaha na Mkuu wa Polisi Jamii mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Michael Manumbu, wakati wa ziara ya kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika katika Kituo cha Kulelea Watoto cha Shallom kilichopo Msangani.

Katika ziara hiyo, askari polisi walijumuika na watoto hao kupitia michezo na chakula cha pamoja, huku wakitoa msaada wa vifaa vya shule, vyakula, na mbuzi wawili kwa ajili ya kituo hicho.

ACP Manumbu amesisitiza kuwa malezi bora ndiyo msingi wa kujenga taifa lenye amani, maadili mema, na lisilo na uhalifu wa baadaye, huku akionya kuwa jeshi hilo halitasita kuwakamata wanaojihusisha na ukatili.

Wakati wa hafla hiyo, watoto walipatiwa elimu ya jinsi ya kujilinda na kuripoti ukatili kwa viongozi na polisi pindi wanapofanyiwa vitendo vibaya.

Msimamizi wa kituo hicho, Lilian Mbise, amelishukuru kwa dhati Jeshi la Polisi kwa upendo, msaada, na moyo wa ubinadamu walio uonesha kwa watoto hao wenye uhitaji maalum.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITVEXTRA >>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *