Dar es Salaam. Mwigizaji na mtayarishaji wa maudhui mtandaoni Idrisa Shabani ‘Anko Mafix’ amesema jina lake la kisanii limetokana na tabia yake ya zamani ya kusimulia hadithi za kubuni. Hali iliyowafanya marafiki zake kumpachika jina hilo ambalo baadaye likawa utambulisho wake katika tasnia ya burudani.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Anko Mafix amesema jina hilo linamaanisha mtu anayependa kutunga visa au hadithi za kuburudisha.

“Marafiki zangu ndio walionipa jina la Anko Mafix, kwa sababu nilikuwa napenda kupiga stori ambazo wao waliziita za mafix. Baadaye likawa jina ambalo kila mtu alinijua nalo,” amesema.

Mafix amesema kipaji chake cha kusimulia hadithi kilianza kuonekana tangu akiwa shule. Ambapo wanafunzi wenzake walikuwa wakifurahia simulizi zake hadi kumpa fedha ili awaelezee hadithi mpya.

Amesema umaarufu wake shuleni ulifanya walimu wafahamu tabia yake ya kusimulia hadithi za kuburudisha.

Ameongezea alipomaliza shule, aliendelea kuwaburudisha watu mtaani kabla ya kujiunga na kundi la sanaa.

“Nilipoacha sanaa nilijaribu kukaa pembeni. Lakini kila mara nilikuwa najikuta nikiambiwa na moyo wangu kwamba nirejee kuigiza,” amesema.

Amesema mwanzo wake rasmi kwenye mitandao ya kijamii ulitokana na video aliyoposti usiku mmoja baada ya kurekodiwa na mke wake.

“Nilipoamka asubuhi nilikuta watu wengi wameitazama video ile. Wameanza kunifuatilia na wengine walikuwa wakiniomba niendelee kuweka kazi nyingine,” amesema.

Anko Mafix amesema sehemu kubwa ya maudhui yake imejikita kwenye masuala ya ndoa kwasababu anaamini jamii inahitaji elimu zaidi kuhusu mahusiano ya kifamilia.

“Napenda kuzungumzia ndoa kwa sababu najua mambo mengi kuhusu upande huo natamani watu wajifunze. Siku hizi hata wanaume wanatoa siri za ndoa nje ya nyumba,” amesema.

Mwigizaji na mtayarishaji wa maudhui mtandaoni Idrisa Shabani ‘Anko Mafix’ amesema jina lake la kisanii limetokana na tabia yake ya zamani ya kusimulia hadithi za kubuni. Hali iliyowafanya marafiki zake kumpachika jina hilo ambalo baadaye likawa utambulisho wake katika tasnia ya burudani.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi Scoop, Anko Mafix amesema jina hilo linamaanisha mtu anayependa kutunga visa au hadithi za kuburudisha.

“Marafiki zangu ndio walionipa jina la Anko Mafix, kwa sababu nilikuwa napenda kupiga stori ambazo wao waliziita za mafix. Baadaye likawa jina ambalo kila mtu alinijua nalo,” amesema.

Mafix amesema kipaji chake cha kusimulia hadithi kilianza kuonekana tangu akiwa shule. Ambapo wanafunzi wenzake walikuwa wakifurahia simulizi zake hadi kumpa fedha ili awaelezee hadithi mpya.

Amesema umaarufu wake shuleni ulifanya walimu wafahamu tabia yake ya kusimulia hadithi za kuburudisha.

Ameongezea alipomaliza shule, aliendelea kuwaburudisha watu mtaani kabla ya kujiunga na kundi la sanaa.

“Nilipoacha sanaa nilijaribu kukaa pembeni. Lakini kila mara nilikuwa najikuta nikiambiwa na moyo wangu kwamba nirejee kuigiza,” amesema.

Amesema mwanzo wake rasmi kwenye mitandao ya kijamii ulitokana na video aliyoposti usiku mmoja baada ya kurekodiwa na mke wake.

“Nilipoamka asubuhi nilikuta watu wengi wameitazama video ile. Wameanza kunifuatilia na wengine walikuwa wakiniomba niendelee kuweka kazi nyingine,” amesema.

Anko Mafix amesema sehemu kubwa ya maudhui yake imejikita kwenye masuala ya ndoa kwasababu anaamini jamii inahitaji elimu zaidi kuhusu mahusiano ya kifamilia.

“Napenda kuzungumzia ndoa kwa sababu najua mambo mengi kuhusu upande huo natamani watu wajifunze. Siku hizi hata wanaume wanatoa siri za ndoa nje ya nyumba,” amesema.

Ameongeza kuwa amekuwa akipokea pongezi kutoka kwa watu mbalimbali wanaodai kufaidika na mafunzo na ujumbe anaoutoa kupitia maudhui yake.

Akizungumzia tofauti yake na watayarishaji wengine wa maudhui, amesema hujikita katika kuonyesha hali halisi ya maisha ya watu wa kawaida.

“Maudhui yangu mengi yanatokana na maisha niliyopitia. Nimeishi mazingira mbalimbali na ndiyo yamenifanya niwe mtunzi mzuri wa hadithi na maigizo,” amesema.

Kupitia sanaa amesema amefanikiwa kujenga na familia yake kuishi vizuri

Hata hivyo, amesema moja ya changamoto kubwa alizowahi kukutana nazo ni katika mahusiano. Akieleza baadhi ya wanawake wamekuwa wakihofia umaarufu wake unaweza kusababisha kuwaacha siku zijazo.

Mbali na changamoto hizo, amesema umaarufu umemletea manufaa mengi ikiwamo kuaminika zaidi na watu. Kujenga mtandao mpana wa mahusiano na kurahisisha baadhi ya mambo katika maisha yake ya kila siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *