
Ujumbe huo umetuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, marafiki na wafanyakazi wenzake na marehemu.
UN yatoa dola milioni 4 kupambana na Ebola Uganda
Wakati huohuo Umoja wa Mataifa umetenga dola milioni nne za Marekani kuisaidia Uganda kukabiliana na mlipuko wa Ebola na kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo. Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, Tom Fletcher amesema fedha hizo kutoka Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF, zitasaidia huduma za afya, ulinzi na usafirishaji katika wilaya 29 zilizo katika hatari kubwa.
Msaada huo pia utaimarisha maandalizi, ufuatiliaji wa ugonjwa na hatua za haraka za kukabiliana na Ebola nchini humo.
Vita dhidi ya Ebola ni mapambano ya kila siku
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani, WHO, limesema uratibu wa kila siku ni muhimu katika kudhibiti mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Kila asubuhi, timu za shirika hilo na wau zinazosaidia hatua za kudhibiti Ebola hukutana kutathmini hali ya ugonjwa, kupitia shughuli zinazoendelea na kuweka vipaumbele vya operesheni za siku hiyo.
WHO imesema mikutano hiyo husaidia kuhakikisha hatua za haraka, zilizoratibiwa na zenye ufanisi. Shirika hilo limeongeza kuwa katika mlipuko wa Ebola, taarifa sahihi za kitaalamu pekee hazitoshi. “Ujumbe lazima pia uaminiwe na jamii,” limesema shirika la WHO, likisisitiza umuhimu wa kujenga imani ya wananchi katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo.