Idadi ya wagonjwa wa Ebola waliothibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka hadi 896, ikiwa ni pamoja na vifo 232, data ya serikali imebainiha siku ya Alhamisi jioni.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Idadi hiyo iliwakilisha jumla ya wagojwa waliothibitishwa kufikia siku ya Jumatano, kulingana na ripoti ya hali iliyorekodi wagonjwa wapya 21 na vifo vipya sita katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Maafisa wa afya wamesema katika ripoti hiyo kwamba kumekuwa na ongezeko la wagonjwa waliothibitishwa wiki baada ya wiki, na hivyo kuendelea kwa maambukizi ya jamii.

Walmeonya kwamba mlipuko huo unaweza kuenea kwa kasi katika maeneo mapya ikiwa hatua za afya ya umma hazitatekelezwa haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *