LONDON, UINGEREZA: Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Uingereza, Sir Lindsay Hoyle, katika makazi rasmi ya Spika leo Juni 18, 2026.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Uingereza, hususan katika nyanja za elimu, biashara, uwekezaji, sayansi na teknolojia, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kibunge kati ya nchi hizo mbili.

Katika kikao hicho, Balozi Kairuki alimueleza Spika kuhusu maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) utakaofanyika Arusha Oktoba 2026.

Spika huyo alieleza kuunga mkono mkutano huo na kusisitiza dhamira yake ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kibunge kati ya Tanzania na Uingereza.

SOMA: Prof. Mkumbo rasmi kusaka wawekezaji Uingereza

Mazungumzo hayo yalidhihirisha uendelevu wa uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Uingereza, pamoja na dhamira ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano wenye manufaa kwa wananchi wa nchi zote mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *