Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema wakati mizozo ikiendelea kushamiri duniani, idadi kubwa ya watoto wa kike na wa kiume wanaendelea kuwa waathirika wa ubakaji, utumwa wa kingono, ndoa za kulazimishwa na biashara haramu ya binadamu.

Watoto wengi wanakumbwa na ukatili huu wa kinyama wakati wa mashambulizi kwenye makazi yao au wanapokuwa wanakimbia vurugu,” amesema.

Ameongeza kuwa baadhi ya watoto hutekwa nyara au kulazimishwa kujiunga na makundi yenye silaha, huku wengine wakilazimishwa kushuhudia au hata kutenda vitendo vya ukatili wa kingono.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema ukatili wa kingono dhidi ya watoto si ajali ya vita. Ukatili wa kingono dhidi ya watoto ni mkakati wa makusudi unaotumika kuadhibu jamii na kuvunja mahusiano ya kijamii.” 

© UNICEF/Vlad Sokhin Msichana mwenye umri wa miaka 13 ambaye hapo awali alishirikihwa kwa kundi la silaha la wapiganaji wa silaha, anashikilia silaha bandia wakati wa sherehe ya ufunguzi wa kituo cha mafunzo na ukarabati katika mji wa Baoro, Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Madhara 

Madhara ya ukatili huo ni makubwa na ya muda mrefu, yanajumuisha majeraha ya mwili, msongo wa mawazo, kisaikolojia pamoja na kutengwa kijamii.

Ili kukomesha ukatili huo kunahitajika hatua katika maeneo matatu muhimu: ulinzi, uwajibikaji na kinga.

Tunahitaji ulinzi ili watoto wawe salama katika maeneo ya mizozo, uwajibikaji ili wahusika wawajibishwe, na kinga kwa kushughulikia mizizi ya ukatili huu,” amesema Guterres.

Kusoma taarifa ya ripoti ya athari zinazowapata watoto katika mizozo bofya hapa

Msaada kwa manusura

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa huduma jumuishi kwa manusura ni muhimu katika kuwasaidia kujenga upya maisha yao na familia zao.

Akihitimisha ujumbe wake, Katibu Mkuu Guterres amesema watoto hawapaswi kamwe kuwa walengwa wa vita. “Kuwalinda watoto ni wajibu wa kisheria na wa kimaadili kwa kila mpiganaji na kila taifa.” amesisitiza.

Ameongeza kuwa licha ya mizozo mingi kuendelea kuwanyima watoto utoto wao, dunia bado ina nafasi ya kujenga mustakabali salama kwa kila mtoto.

“Kwa pamoja tunaweza kujenga dunia ambako kila mtoto wa kike na wa kiume anakua kwa usalama na utu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *