Kahama. Watu sita wamefariki dunia huku wengine watano wakijeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria T985 DXL TATA mali ya kampuni ya OG Classic likitokea Kahama kuelekea mkoani Geita lililoligonga lori kwa nyuma.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba imetokea katika eneo la Wendele Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga leo jumamosi juni 20, 2026, majira ya saa 12 asubuhi.

Kwa mujibu wa kamanda Magomi uchunguzi wa awali chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa basi lililokuwa likitokea Kahama kwenda Geita, aliyejaribu kulipita lori bila kuchukua tahadhari na kisha kugonga ukingo wa barabarani na kurudi kugonga tela la lori, na kisha kupinduka na kusababisha vifo na majeruhi.

Amesema “Dereva wa basi alipofika eneo la Wendele, alilikuta lori ambalo nalo lilikuwa likielekea Masumbwe, alijaribu kulipita bila kuchukua tahadhari huku akiwa katika mwendokasi, ndipo alipogonga ngema na kurudi kuligonga tela la lori kasha kupinduka.”

Majeruhi wa ajali hiyo akiwemo Seni Bundala amesema “Gari letu lilikuwa mwendokasi na abiria walikuwa wakilalamika kwa dereva lakini hakutaka kutusikiliza.”

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *