
Duru ya kwanza ya majadiliano kati ya Marekani na Iran kutafuta amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati imemalizika usiku wa Jumapili Juni 21 kuamkia Jumatatu Juni 22 nchini Uswisi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchi hizo mbili zilikubaliana juu ya suala la kuhitimisha makubaliano ya mwisho ndani ya siku 60. Pia walikubaliana juu ya kuanzishwa kwa “laini ya mawasiliano” ili kupata usafiri katika Mlango-Bahari wa Hormuz na “kiini cha kudhibiti migogoro” ili kukomesha mapigano nchini Lebanon, walitangaza wapatanishi wa Pakistan na Qatar.
Wapatanishi Pakistan na Qatar wanasema Marekani na Iran zimefanya “maendeleo ya kutia moyo” katika siku ya kwanza ya mazungumzo ya ngazi ya juu nchini Uswisi.
Mazungumzo hayo yaligubikwa na suala la kuanzisha mifumo ya mawasiliano ili kuhakikisha kuwa Mlango Bahari wa Hormuz utaendelea kuwa wazi pamoja na mapigano yanayoendelea nchini Lebanon kati ya Israel na Hezbollah. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kumefikiwa “maendeleo makubwa” kuhusu Lebanon, mali za Iran zilizozuiwa pamoja na kuondolewa kwa vikwazo vya mafuta.