f

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba ndege za kivita za Marekani zimeshambulia maghala ya makombora na ndege zisizo na rubani za Iran pamoja na vituo vya rada katika maeneo ya pwani.

Trump amesema mashambulizi hayo yalifanyika kujibu kile alichokitaja kuwa “ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya kusitisha mapigano” na akaonya kwamba ikiwa Marekani italazimika “kukamilisha” operesheni zake za kijeshi, basi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitakuwepo tena.

Kwa upande mwingine, Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC) imetangaza kwamba imelenga vituo vya kijeshi vya Marekani katika kambi ya Ali al Salem nchini Kuwait na makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Jeshi la Wanamaji la Marekani nchini Bahrain kwa kutumia makombora ya masafa marefu na ndege zisizo na rubani.

IRGC pia imeonya kwamba itachukua hatua kali zaidi dhidi ya meli inazozitaja kuwa “zinazokiuka” masharti yaliyowekwa.

Baada ya mashambulizi hayo ya pande zote mbili, Marekani na Iran zilishutumiana kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.

Katika taarifa yake, Centcom ilisema: “Iran ilipewa fursa ya kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano, lakini ilichagua kutofanya hivyo wakati vikosi vyake viliporusha ndege isiyo na rubani ya kujitoa mhanga iliyogonga meli ya mafuta ya MT Kiku,” meli iliyosajiliwa nchini Panama.

Maelezo zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *