
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 36 alikamatwa alipokuwa akiandamana na mtu anayetarajiwa kuajiriwa kwenye kituo cha basi mjini Harare kwa ajili ya usafiri hadi Urusi. Anashutumiwa kwa kuajiri watu watano kwa ajili ya jeshi la Urusi kuhusiana na uvamizi wake katika eneo la Ukraine.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchini Zimbabwe, polisi wa kupambana na ugaidi walitangaza siku ya Jumatatu, Juni 29, kukamatwa na kushtakiwa kwa mtu anayetuhumiwa kwa kuajiri wapiganaji kwa ajili ya kwenda katika vita nchini Ukraine. Kulingana na shirikala habari laAFP, ikinukuu hati za mahakama, mtu huyo mwenye umri wa miaka 36 alikamatwa alipokuwa akiandamana na mtu anayetarajiwa kuajiriwa kwenye kituo cha basi huko Harare kwa safari ya kwenda Urusi kupitia Afrika Kusini.
Mshukiwa alikuwa na visa vya kielektroniki vya Urusi na uthibitisho kadhaa wa kuchukuwa chumba hotelini. Inadaiwa aliajiri jumla ya watu watano, kwa lengo la kuwafanya wasaini mikataba na jeshi la Urusi kuhusiana na mashambulizi nchini Ukraine.
Raia wa Urusi aliyetambuliwa kama mshirika wake bado hajakamatwa, kulingana na polisi wa Zimbabwe iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP.
Kuajiri kwa lazima
Kukamatwa huku si mara ya kwanza kwa aina yake nchini Zimbabwe, nchi yenye uhusiano wa karibu na Moscow. Mwezi Machi mwaka huu, watu wanne walishtakiwa kwa biashara haramu ya binadamu nchini humo, pia wakihusishwa na mtu aliyekuwa akifanya kazi kwa niaba ya Urusi. Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, waathiriwa waliajiriwa kupitia programu za ujumbe mfupi wakiwa na ahadi za kazi za kuzima moto, mishahara mikubwa, na mazingira mazuri ya kazi nchini Urusi. Lakini walipofika, hati zao zilichukuliwa, na walilazimishwa kujiandikisha katika jeshi la Urusi.
Kesi hiyo ilisababisha serikali kuthibitisha vifo vya Wazimbabwe 18 katika mapigano “nje ya nchi,” na uwepo wa zaidi ya watu 60 “wamekwama” nchini Urusi.
Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Urusi vilisambaza video ya mwanajeshi akijitambulisha kama Mzimbabwe na kudai kutendewa vizuri akiwa amevaa sare za Urusi.