Balozi Al-Harith Idriss, ambaye ni mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, na mshauri wa Marekani kwa masuala ya Afrika na nchi za Kiarabu walitofautiana vikali. Mzozo huo unatokana na juhudi za kupata amani na kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Massad Boulos, mshauri mkuu katika Wizara ya Mambo ya Marekani kwa Nchi za Kiarabu na Afrika, na Al-Harith Idriss al-Harith Mohamed, mwakilishi wa kudumu wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, walitupiana maneno kuhusu nia ya Khartoum ya kukubali mapendekezo ya amani katika mzozo kati ya jeshi la serikali la Sudan na wanamgambo wa RSF ulioanza mwezi Aprili 2023.

Taarifa zilizotolewa na Massad Boulos, Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Afrika, mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan zimeikasirisha Khartoum. Boulos alidai mnamo Juni 27, 2026, kwamba Baraza Kuu la Sudan lilikataa mapendekezo yake ya amani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilifafanua matamshi haya, ikisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba madai ya Bw. Boulos “si sahihi” na “hayaonyeshi msimamo halisi wa Khartoum.”

Marekani, kupitia wapatanishi wake, iliwasilisha mapendekezo ya kuleta amani na kusitisha mapigano (truce) ili kusaidia wananchi.

 Mwakilishi wa Khartoum alisema kuwa walitoa jibu chanya. Hata hivyo, alidai kuwa mshauri wa Marekani alishindwa kusoma wala kuzingatia maandishi ya majibu hayo ya Sudan.

Khartoum inajitetea. Khartoum inasisitiza kwamba, tangu mwanzo wa vita, imezingatia mapendekezo yote yanayolenga kukomesha mateso ya watu wa Sudan kwa njia “chanya na ya uwajibikaji”.

Inasema kwamba ilisaini Mkataba wa Jeddah mnamo Mei 2023, ikakubali makualiano kadhaa ya kusitisha mapigano kwa ajili ya kibinadamu, na ikazindua mpango wake wa amani wa Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Desemba 2025.

 Kulingana na balozi wa Sudan, hati waliyoiwasilisha ina kalenda maalum ya kuondoa majeshi na kurudisha amani, lakini Marekani haikuchukua muda kuisoma.

Hali hii inaonesha mabadiliko ya mikakati na mvutano kati ya Washington na jeshi la serikali ya Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *