Watu wenye silaha wamevamia mji huo, ulioko katika mkoa wa Vakaga kaskazini mashariki mwa nchi, alfajiri ya Jumanne, Juni 30, na kuushikilia kwa saa kadhaa. Ingawa idadi ya vifo kutokana na shambulio hilo bado haijulikani katika hatua hii, vyanzo mbalimbali vinalielezea kama shambulio baya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, shambulio baya lililenga mji wa Am Dafok, karibu na mpaka wa Sudan, siku ya Jumanne, Juni 30. Alfajiri, watu wenye silaha walivamia mji huo na kusababisha machafuko, kabla ya wanamgambo wa Urusi Wagner kuanza mashambulizi ya anga.

Kulingana na chanzo cha ndani, washambuliaji walifika kutoka nchi jirani ya Sudan asubuhi na mapema na kudhibiti mji huo hadi alasiri, ambapo milio ya risasi iliendelea kusikika. Mamlaka za eneo hilo na baadhi ya wakazi walitafuta hifadhi karibu na kambi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), ambacho pia kilikuwa kikilengwa. Walinda amani watatu kutoka kikosi cha Zambia walijeruhiwa, mmoja wao alijeruhiwa vibaya.

Katika taarifa yake, ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulilaani shambulio hilo la muungano wa wanajeshi kutoka kundi la waasi wa Popular Front for the Renaissance of the Central African Republic (FPRC) linaloongozwa na Noureddine Adam, kundi la waasi la MDRP) linaloongozwa na Arda Hakouma, na makundi mengine yenye silaha “yasiyojulikana”.

Shambulio la anga

Kwa kuwa mtandao wa simu ulikatawa, ilikuwa vigumu kupata tathmini ya vifo vya raia Jumanne jioni, lakini chanzo cha ndani kilichowasiliana na RFI huko Birao, mkoa wa Vakaga, kilithibitisha kwamba kulikuwa na vifo kadhaa—ikiwa ni pamoja na maafisa wa polisi—na majeruhi wengi. Karibu nyumba thelathini pia ziliripotiwa kuchomwa moto na kuporwa.

Ingawa makao makuu ya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati haikutoa hesabu ya majeruhi, ilidai kwamba shambulio la angani liliwatawanya maadui, ambao “wanajificha” miongoni mwa raia nchini Sudan.

Kwa upande wake, msemaji wa muungao wa makaundi hayo ya waasi unaoitwa Muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko ya Msingi (CPC-F), Aboubacar Sidick Ali, alidai kuwaua watu zaidi kumi katika kambi ya serikali na kwamba waliendelea kuchukuwa udhibiti wa mji wa Am Dafok hadi jioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *