
Rais wa Marekani Donald Trump amerekodi takriban dola bilioni 1.2 kutokana na shughuli zake za sarafu za kidijitali mwaka wa 2025, kulingana na hesabu za shirika la habari la AFP kupitia hati zilizochapishwa siku ya Jumanne na Ofisi ya Maadili ya Serikali (OGE).
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Sheria ya mwaka 1978 inamtaka rais wa Marekani na makamu wa rais kutangaza mapato na mali zao. Kulingana na kurasa 927 za hati zilizotolewa kwa umma, rais alipokea karibu dola milioni 550 (euro milioni 482) kutokana na uhusiano wake na shirika jipya la World Liberty Financial (WLF). Jukwaa hili la sarafu za kidijitali lilianzishwa pamoja mnamo mwezi Septemba 2024 na watoto wa Donald Trump na mtoto wa mjumbe wa Marekani Mashariki ya Kati, Steve Witkoff.
Kulingana na nyaraka rasmi zilizochapishwa hivi karibuni na Ofisi ya Maadili ya Serikali ya Marekani (OGE), Rais Donald Trump alipokea takriban dola bilioni 1.2 kutokana na shughuli zake na familia yake za sarafu za mtandao.
Alipokea takriban dola milioni 550 kutoka kwa kampuni ya sarafu ya mtandaoni inayoitwa WLF, ambayo yeye na wanawe walianzisha.
Alipata takriban dola milioni 635 kama mrabaha kutokana na leseni ya sarafu ya mtandao inayotumia jina lake.
Mapato mengine yalitokana na mauzo ya sehemu ya hisa za kampuni hiyo katika masoko ya kimataifa, kama vile uwekezaji kutoka Mashariki ya Kati.
Mafanikio haya ya kifedha katika ulimwengu wa kidijitali ndiyo sababu kuu iliyofanya utajiri wake wa kibinafsi kukua kwa haraka na kufikia dola bilioni 6.5.