
ILIPOISHIA
Aliposindika mlango aliifungua shuka yake aliyokuwa amejifunga na kuitupa chini. Sikutaka hata kumtazama. Na mimi nikasimama na kugeuka upande mwingine. Nikaanza kupembua nguo zangu moja baada ya nyingine.
Nilikuwa nimelazimika kufanya kitendo ambacho moyo wangu ulikuwa haukitaki. Lakini moyo huo huo ukaniambia. “potelea mbali”
SASA ENDELEA…
Nilimaliza kuvua nguo zote na kuziweka chini, nikabaki na nguo ya ndani. Hapo nilijishauri sana kama niivue au nisiivue. Niliwaza kwamba nikiivua, shanga zangu ataziona. Lakini si shanga tu, kuna mengi makubwa atakayoyaona!
Nikageuka na kumtupia jicho mara moja tu kisha nikageuza uso wangu. Alikuwa amesimama nyuma yangu akinitazama huku ameshika jitunguri kubwa mikononi. Alikuwa mtupu kama alivyozaliwa!
“Nakusubiri wewe,” akaniambia.
Ndipo nilipoishika ile nguo ya ndani na kuisukuma chini. Kimoyomoyo nilijiambia sitageuka tena upande wake na macho yangu nitayafumba.
Nilipoitupa chini nguo yangu ya ndani, nikabaki nimesimama vilevile nimempa mgongo.
“Geuka huku,” sauti yake ikanishitua.
Nilishamwelewa, lakini kwa kiwewe nilichokuwa nacho nikamuuliza:
“Nigeuke wapi?”
“Geuka huku kwangu.”
Aliponiona nasita, alinishika bega na kunigeuza. Nikafumba macho. Sikutaka kutazamana naye.
“Fumbua macho yako,” akaniambia.
Nikayafumbua na kuangalia upande mwingine.
“Chuchumaa.”
Nikachuchumaa. Yeye alikuwa amesimama. Sasa fikiria mwenyewe vile nilivyokuwa mkabala naye na tukiwa karibu, kitu chake gani kilikuwa juu ya kichwa changu!
Akaiweka tunguri yake juu ya kichwa changu kisha akaniuliza:
“Mume wako anaitwa nani?”
“Mashaka.”
Akalitaja jina hilo kisha akaniuliza:
“Na wewe unaitwa nani?”
“Naitwa Sharifa.”
Akaanza kutabana maneno kwa lugha ya kikwao huku akilitaja jina la Mashaka na jina langu. Wakati akitabana alikuwa akiigonga ile tunguri kwenye kichwa changu. Alifanya hivyo kwa karibu robo saa.
Akaja upande wa nyuma yangu akafanya hivyo hivyo. Baada ya hapo niliona akifungua kiwembe. Kwa vile sikujua kama kiwembe hicho kilikuwa kipya au cha zamani, nikamuuliza:
“Baba, hicho kiwembe ni kipya?”
“Ndiyo, nakifungua sasa kwenye karatasi. Nikishamchanjia mtu ninakitupa. Najua kuwa kuna matatizo. Mara kwa mara tunaitwa kwenye semina na kuambiwa tusiwachanjie watu wawili kwa kiwembe kimoja.”
Mganga akaanza kunichanja. Kwanza alinichanja kwenye paji la uso wangu. Kisha akaniambia nitoe ulimi wangu. Nilipoutoa akauchanja.
“Sasa kaa chini kisha ulale chali.”
Aliponiambia hivyo nilishtuka. Nikamuuliza:
“Umesema nilale chali?”
“Ndiyo. Lala chali.”
Nikalala, lakini miguu yangu niliibana kwa nguvu. Nikajiambia kama atathubutu kunifanyia mzaha wowote nitapiga kelele.
Mganga naye akachutama. Nikaona mkono wake ukielekea chini ya kitovu changu.
Akanichanja chini ya kitovu, kisha akanichanja juu ya mguu wangu wa kulia na wa kushoto.
Baada ya hapo akaanza kunipaka dawa iliyotoka kwenye ile tunguri. Wakati ananipaka alikuwa akiimba nyimbo za kiganga za kikwao.
Alipomaliza aliniambia:
“Inuka.”
Nikainuka.
“Nivae nguo zangu?”
“Mbona una haraka?”
“Nauliza tu.”
Akanyamaza kimya. Alichukua tunguri nyingine akautia ule mchanga wa alama za viatu vya Mashaka pamoja na zile nyuzi za suruali yake. Akavitabania maneno ambayo sikuyaelewa.
Baada ya hapo aliumimina ule mchanga na zile nyuzi kwenye kikaratasi. Vilikuwa vimechanganyika na dawa ya mafuta mazito iliyokuwa ndani ya tunguri hiyo.
Kulikuwa na chetezo kilichokuwa karibu yake, akakichukua na kufungua mlango kidogo na kukitoa kile chetezo huku akipaza sauti yake:
“Lete moto!”
Nikasikia hatua za mtu huko uani akija pale mlangoni, akakichukua kile chetezo. Baada ya muda kidogo, chetezo kilirudishwa kikiwa na makaa ya moto. Kilipenyezwa ndani. Mganga akakichukua kisha akaubana tena mlango.
Alikiweka kile chetezo mbele yangu kisha akaniambia niichukue ile karatasi iliyokuwa na dawa zake alizozitoa kwenye ile tunguri, niitie kwenye ule moto.
Nikafanya kama alivyoniambia. Nikaona moshi unatoka.
“Sasa nuia vile unavyotaka kwa mume wako.”
“Ninuie kwa sauti inayosikika au kimya kimya?” nikamuuliza.
“Unavyotaka mwenyewe.”
“Nitanuia kimya kimya,” nikamwambia kisha nikaanza kunuia kama nilivyoambiwa.
Nilinuia mengi kuhusu mume wangu.
Nayakumbuka baadhi ya maneno niliyonuia. Nilisema hivi:
“…nataka huyu mwanaume aachane na huyo mwanamke wake, amuone kama kinyesi cha binadamu, na pia asitamani mwanamke mwingine yeyote. Anipende na kunitamani mimi peke yangu. Kila nitakachomwambia mimi anikubalie. Nikitaka pesa anipe bila kuniuliza maswali…”
Nilipomaliza manuizi yangu nikamtazama yule mganga.
“Tayari.”
“Sawa. Sasa lala tena tutengeneze utamu,” akaniambia.
Nikalala tena chali, miguu yangu nikiwa nimeibana.
“Usibane miguu,” akaniambia.
Kwenye kiganja cha mkono wake wa kushoto alikuwa ameweka vitone vya mafuta.
Nikaacha kuibanisha miguu yangu, lakini nilikuwa nimemtolea macho.
“Ichanue kabisa,” akaniambia.
Nikaguna kisha nikaichanua kidogo. Sasa alikuwa akiona kwa uwazi kile ambacho nilitaka asikione.
Akaanza kunipaka yale mafuta mahali pale pale ambapo nilikuwa sitaki paonekane. Ninavyojua mimi, mafuta hupakwa kwa kiganja, lakini yule baba alikuwa akitumia vidole.
Macho yangu yalikuwa yakimtazama usoni kwake. Nilijiambia kama alikuwa na dhamira mbaya nitamgundua kwenye uso wake.
Nikamsikia akisema:
“Hii dawa ninayoipaka hapa, huyu mume wako akikutana nawe usiku kwenye sita kwa sita achanganyikiwe kuliko kawaida. Hata akienda kwa mwanamke mwingine aone ovyo. Ampe kila anachotaka mke wake….”
Wakati mganga akisema hivyo, mimi nilikuwa nikiitikia, “Ndiyo… ndiyo… ndiyo…”
Kucha zake zilikuwa zikiniumiza, lakini nilijikaza tu.
Baada ya hapo akaanza kunipaka yale mafuta kwenye mapaja. Alipotoka kwenye mapaja akaja kwenye kiuno na tumbo. Wakati ananisugua alikuwa akizigusa gusa shanga zangu.
Akapandisha mikono yake hadi kwenye matiti yangu. Matiti pia yalisuguliwa. Huko kote alikuwa akinisugua haraka haraka, lakini alipofika kwenye yale matiti, mikono yake ilichukua muda mrefu.
Sasa kulikuwa na kitu kingine ambacho nilikuwa ninakiona katika hisia zangu. Alivyokuwa akinipaka ile dawa kwenye mapaja na kwenye matiti, nilikuwa nahisi hali ya kutamani tendo la ndoa. Kadiri alivyokuwa akinisugua, ndivyo nilivyoisikia hali hiyo kwa nguvu, hasa mikono yake ilipokuwa kwenye ncha za matiti.
Mwili ukiwa umenilegea, nilijiuliza, *huyu baba ananipaka dawa gani jamani?*
Nikauhisi mwili wangu ukiwa mzito kiasi kwamba hata angeniambia ninyanyuke pale pale, ingekuwa shida. Yaani ilibaki kidogo tu nimwambie, “Baba nisaidie hicho kitu, niko taabani…”
Lakini niliendelea kujikaza. Uso wangu niliuelekeza upande mwingine ili asiyaone macho yangu na kugundua hali niliyokuwa nayo.
“Baba, maliza basi, unaniumiza…” nikamwambia yule mganga kimoyomoyo baada ya kuona alikuwa anachelewa.
Niliogopa kutoa sauti. Na hata kama nisingeogopa kutoa sauti, nguvu ya kumwambia hivyo pia sikuwa nayo. Nilikuwa hoi kabisa.
“Haya, inuka,” nikaisikia sauti yake kwa mbali.
Nikajiinua. Bila shaka alijua nilikuwa katika hali gani kwani alikuwa akinitazama machoni mwangu.
“Sasa vaa nguo zako,” akaniambia.
Jamani, baadhi ya waganga wa kienyeji wanaona mengi. Kama ndivyo wanavyowachezea wake za watu, sitakubali wifi yangu aende kwa mganga.
Nikakusanya nguvu zangu na kuinuka. Nikavaa nguo zangu haraka haraka. Uso wangu ulikuwa umetahayari kama vile nilifumaniwa na mwanaume. Kile kitendo kilichopita kilikuwa kama nimetembea na mwanaume.
Baada ya kuvaa akaniambia:
“Hutakiwi tena kukaa chini, nipe malipo uende zako. Baada ya siku tatu njoo tena.”
Nikatoa ile pesa yake aliyoniambia jana yake. Wakati nampa nikakumbuka kwamba anataka iwekwe chini, nikaiweka chini.
“Ni kiasi gani?” akaniuliza.
“Ni shilingi laki moja.”
“Sawa. Sasa nisikilize kwa makini. Leo usioge na uhakikishe kwamba unachanganyika naye usiku, lakini kuwe na giza.”
“Sawa,” nikamkubalia.
“Hakuna dawa ya kumtilia kwenye chakula?”
“Ukija siku hiyo ya tatu ndiyo nitakupa dawa hiyo. Siwezi kutoa dawa zote kwa pamoja, zinaweza kumchanganya akili.”
“Sasa lini ataanza kubadilika?”
“Haitachukua muda. Utaanza kuona mabadiliko kidogo kidogo, lakini siku utakapokuja nikikupa hiyo dawa ya kumtilia kwenye chakula ndiyo utaona mabadiliko makubwa. Utamuona haondoki nyumbani na kila wakati anataka kuwa na wewe.”