Spika: Nchi haiwezi kujengwa kwa maandamanoSpika: Nchi haiwezi kujengwa kwa maandamano

DAR ES SALAAM; Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu, amesema nchi haiwezi kujengwa kwa maandamano na kwamba amani ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Ametoa kauli hiyo Dar es Salaam leo kwenye mkutano wake na wahariri kuhusu maadhimisho ya miaka 100 ya chimbuko la Bunge la Tanzania na kueleza kuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa kuhusu demokrasia, ikiwa ni pamoja na kuwafungulia milango baadhi ya wanasiasa waliokuwa wamekimbilia nje ya Tanzania kurejea nchini.

Ameseman chi haiwezi kujengwa kupitia maandamano, wala haiwezi kujengwa kwa watu kushutumiana na kueleza kuwa yapo mambo mazuri ambayo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia imefanya na yanastahili pongezi kuanzia miundombinu, demokrasia na hata utawala bora.

Kuhusu maadhimisho amesema wanachoangalia ni chimbuko la bunge hilo kuanzia lilipoanzishwa Machi 19, 1926, wakati nchi ikiitwa Tanganyika ikiwa koloni la Uingereza, hadi ilipopata uhuru mwaka 1961 na baadaye kuungana na Zanzibar na kuzaliwa Tanzania mwaka 1964.

Amesema bunge la ukoloni lilizinduliwa rasmi Oktoba 10, 1926 na kuanza kufanya kazi zake Desemba mwaka mwaka huo na kueleza kuwa matukio mbalimbali yatafanyika katika maadhimisho ya miaka hiyo 100 na kilele chake kitakuwa Januari 2027.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *