Zaidi ya wakazi 280,000 wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanatarajiwa kunufaika na mradi wa kisasa wa maegesho ya magari uliojengwa katika Kata ya Lilambo kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kupanua miundombinu ya mji huo unaokua kwa kasi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Lilambo, Tea Komba, amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Machi 1, 2025 na kugharimu shilingi bilioni 1.027.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Lilambo B amesema mradi huo umewanufaisha wananchi kwa kutoa ajira wakati wa ujenzi na unatarajiwa kuendelea kufungua fursa za biashara na kuongeza kipato kwa wakazi wa eneo hilo.
Baadhi ya wananchi wa Lilambo, akiwemo Joyce Elia na Mzee SK, wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka mradi huo, wakieleza kuwa utachochea maendeleo ya kiuchumi, kuongeza shughuli za biashara na kuwapa vijana hamasa ya kujiajiri na kutafuta kipato.
(Feed generated with FetchRSS)