Mabalozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, EU) huko Brussels wanajadili leo Ijumaa, Julai 10, uwezekano wa kuzuia uagizaji wa bidhaa kutoka maeneo yanayokaliwa na walowezi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa. Tume ya Ulaya ilituma chaguzi kadhaa kwa nchi hizi wanachama wa Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tume ya Ulaya inapendekeza njia tatu za kuzuia uagizaji wa bidhaa kutoka maeneo yanayokaliwa na Waisrael katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, anaripoti mwandishi wetu huko Brussels, Pierre Bénazet. Chaguo la kwanza itakuwa kutekeleza marufuku ya uingizaji wa sehemu au jumla, sawa na hatua zilizochukuliwa na Uhispania na Ireland.

Chaguo la pili linarudia pendekezo la Ufaransa na Sweden lililowasilishwa mwezi Aprili mwaka huu: kuanzisha leseni za usafirishaji nje. Hata hivyo, Tume inabaini kwamba mfumo kama huo ungekuwa rahisi kukwepa, kwani walowezi wa Israel tayari wanafanikiwa kuleta bidhaa zao katika EU kwa kuziwasilisha kama bidhaa za Israel. Chaguo la tatu litakuwa kutoza ushuru mkubwa, lakini Tume inabainisha kuwa Israel tayari inatoa punguzo kwa walowezi, ambalo lingepunguza ufanisi wa hatua kama hiyo.

Asili ngumu kufuatilia

Kwa nchi za Umoja wa Ulaya, maeno yanayokaliwa na walowezi yanachukuliwa kuwa kinyume cha sheria chini ya sheria za kimataifa, maazimio ya Umoja wa Mataifa, na maoni ya ushauri yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki mnamo mwaka 2024. Bidhaa kutoka maeneo hayo tayari zimetengwa katika Mkataba wa ushirika wa EU na Israel. Hata hivyo, kwa sababu asili yao ni ngumu kutambua, bado bidha hizo zinafikia soko la Ulaya.

Tume inabaini kwamba njia itakayochaguliwa itatumika chini ya sera ya kigeni, ambayo itahitaji kura ya pamoja. Hadi sasa hili limeonekana kuwa haliwezekani kufanikisha, kama ilivyokuwa kwa faili iliyositishwa, hata kwa sehemu, kwa Mkataba wa ushirika wa EU na Israel. Mwakilishi Mkuu wa EU wa Sera ya Mambo ya Nje na Usalama, Kaja Kallas, anatetea hatua inayotegemea biashara pekee, ambayo itahitaji tu kura ya wengi.

Israel inashikilia Ukingo wa Magharibi tangu mwaka 1967, eneo la Palestina ambapo zaidi ya walowezi 500,000 wa Israel wanaishi miongoni mwa karibu Wapalestina milioni tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *