
Kwa nini JozaniAI
Chapisho la UNDP linasema sekta ya utalii inachangia takribani asilimia 50 ya Pato la Taifa la Zanzibar (GDP) na inasaidia ajira zipatazo milioni 1.6. Hata hivyo, watunga sera walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa: tafiti za kila mwaka zinazofanywa kwa watalii wanapoondoka nchini ziliacha pengo la siku 364 bila taarifa mpya, huku zaidi ya maoni 100,000 yanayowekwa kila mwaka na watalii kwenye majukwaa makubwa ya mtandaoni ya kuhifadhi safari na malazi (Online Travel Platforms – OTPs) yakibaki bila kuchambuliwa.
Je inafanya hivi kazi JozaniAI?
JozaniAI ni teknolojia inayotumiwa na serikali kuchambua maoni ya watalii . Kila hoteli na wavuti mbalimbali zina mifumo ya kuwezesha wahudumiwa kutoa maoni. Hii ilikuwa vigumu kwa serikali kupitia kila wavuti. Na huduma nyingine hazikuwa na mifumo ya maoni. Kama uwanja wa ndege ni fomu zilikuwa zinajazwa na zilikuwa ni nyingi sana.
Sasa serikali inatumia apu ya JozaniAI kuangalia hayo maoni na kuona watalii wanasema nini, iwe huduma changamoto kwenye kifungua kinywa, au kwenye usafiri au kwenye uwanja wa ndege.
Programu hii imetumika kwa mwaka mmoja sasa na inaendelea kuboreshwa wakati ambapo UNDP Tanzania kufuatia ombi la serikali ya Zanzibar, inaangalia jinsi ya kupanua huduma hii katika sekta nyingine kama vile kilimo.
« Serikali ya Zanzibar imefurahi sana na manufaa ya JozaniAI kwa jinsi imeboresha huduma. Tunataka kuangalia sekta nyingine kama kilimo, kusaidia wakulima kuchagua mimea na kuangalia bei kule wanakotaka kuuza bidhaa zao. »
Mfano wa manufaa ya JozaniAI katika huduma
Kwa mfano huduma za usafiri imetumika vizuri . Watalii wanatumia aina mbalimbali za usafiri kama magari, bodaboda. “Lakini unapata kuna wakati wanakuwa wana malalamiko kulingana na pengine hawajui ni dereva gani. Pengine gari linakuja si gari zuri, si gari safi. Kama unakuta lile gari wameitisha likifika linakuwa ni gari tofauti . Serikali imeweza kujua na kuchukua hatua jinsi ya kusimamia.”
Je kwa mwananchi wa kawaida?
Sekta ya utalii ikiendelea kuwa kubwa ndio inaajiri watu wengi hasa vijana na wanawake, wanapata kazi na wanapata riziki yao. “Kwa hiyo vile inaendesha uchumi, ndio kila mtu anaweza kupata riziki.”
Vipi JozaniAI na utunzaji wa taarifa binafsi?
Kuna sheria ya Tanzania na Zanzibar ya kutunza taarifa binafsi na hilo ni muhimu sana. “JozaniAI na majukwaa yote ya mitandao ambako watalii wanaweka maoni yao yanazingatia sheria hiyo. Kwa hivyo hakuna maoni yako binafsi ama data yako binafsi itachukuliwa na kuwekwa hadharini. Na pia haiwezi kutambulisha wewe mtoa maoni ni nani.”