Ikitolewa leo Geneva, USwisi na New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN Women, ripoti hiyo imepatiwa jina Zaidi ya Kiwango cha Kuvumilika.

Changamoto kuu

  • Zaidi ya wanawake na wasichana milioni 120 duniani wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi.
  • Asilimia 84 ya mashirika ya wanawake yameripoti kuongezeka kwa mahitaji ya huduma, lakini takribani asilimia 90 ya mahitaji hayawezi tena kuyakidhi.
  • Mashirika 2 kati ya 5 yanatarajia kufungwa ndani ya mwaka mmoja kutokana na ukosefu wa fedha.
  • Zaidi ya watu bilioni 1 wanaishi katika mazingira ya migogoro na umaskini, huku ukatili wa kijinsia na idadi ya wasichana wanaoacha shule ikiongezeka.
  • Huduma muhimu kama hifadhi salama, huduma za afya na msaada kwa manusura wa ukatili wa kijinsia zimepungua kwa kiasi kikubwa

Sofia Calltorp, ambaye ni Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu katika UN Women akizungumzia hali hii amesema, “mashirika ya wanawake yaliyo katika hatari ya kufungwa ndiyo yaliyopo mstari wa mbele katika majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani. Katika nchi kama Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Haiti, yanafanya kazi katika maeneo ambayo wahudumu wa kimataifa hawawezi kufika na huendelea kuhudumia jamii hata baada ya dunia kuhamishia umakini wake kwingine. Kila dola inayokatwa kutoka kwa mashirika haya ni dola inayonyimwa manusura wa ukatili wa kingono unaotokana na migogoro, akina mama waliokimbia makazi yao, wasichana waliolazimika kuacha shule na jamii zinazopambana kuendelea kuishi,”

Mapendekezo ya UN Women

  • Kuongeza na kuendeleza uwekezaji katika mashirika yanayoongozwa na wanawake.
  • Kuhakikisha huduma za kuokoa maisha kwa wanawake na wasichana zinaendelea kutolewa bila kukatizwa.
  • Kuimarisha ulinzi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na wanawake waliokimbia makazi yao.
  • Kuwekeza katika uongozi wa wanawake na usawa wa kijinsia kama sehemu ya kujenga amani na kuleta nafuu baada ya migogoro.
  • Kushirikiana na mashirika ya wanawake kama wadau muhimu katika kutoa misaada ya kibinadamu na kujenga ustahimilivu wa jamii.

Soma ripoti nzima hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *