
Nchini Afrika Kusini, wageni wanaendelea kuondoka kwa wingi nchini humo, kwa hiari au kufukuzwa. Kamati ya wizara inayohusika na uhamiaji ilitangaza siku ya Jumapili Julai 12, 2026 kwamba zaidi ya watu 53,000 wamefukuzwa na kurejeshwa makwao katika wiki za hivi karibuni, hasa raia wa Malawi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Josephine Kloeckner
Mvutano, ambao ulishika kasi wakati wa maandamano mnamo Juni 30, umepungua kwa kiasi fulani, lakini makundi yanayopinga wahamiaji yanaendelea, mara kwa mara, kuandamana na kufanya operesheni za nyumba kwa nyumba kuwasaka wahamiaji haramu.
Katika mkutano mrefu, mawaziri wanaohusika na masuala ya uhamiaji walitoa taarifa mpya kuhusu operesheni za kuwafukuza raia wa kigeni. Mmamoloko Kubayi, Waziri wa Sheria, alisema, “Kituo cha muda cha kuwashughulikia wahamiaji kimeanzishwa Musina na kilianza shughuli Julai 1, 2026. Zaidi ya raia wa kigeni 20,000 wamerejeshwa kupitia kituo hiki.”
Mashambulizi dhidi ya nyumba za raia wa kigeni
Kwa jumla, zaidi ya wageni 53,000 wamefukuzwa au kurejeshwa na serikali zao. Congo-Brazzaville hivi karibuni ilijiunga na nchi nyingi ambazo zimekodi ndege katika miezi ya hivi karibuni na kuwawarudidha nyumbani zaidi ya raia 150 mapema mwezi Julai. “Ninapozungumza nanyi, bado tunawasajili ndugu zetu,” anasema Jurol Loemba, mwanaharakati na mjumbe wa Kamati ya kuwarejesha nyumbani raia wa Kongo kutoka Afrika Kusini. Analaumu vitendo vinavyoendelea vya kujichukulia sheria mkonoi. “Bado tunashuhudia baadhi ya makundi yanaendelea kufanya mashambulizi kwenye nyumba za wageni. Bado tunarekodi visa vya watu kushambuliwa wakati wa maandamano haya.”
Mamlaka imewaonya Waafrika Kusini kwamba vitendo kama hivyo vitakuwa na athari, ingawa polisi hadi sasa hawajaingilia kati sana. Tangu Juni 30, takriban maandamano ishirini yamerekodiwa kote nchini.