
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika barua rasmi kwa Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Vilevile imesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa sheria za kimataifa za kibinadamu, kulindwa wafanyakazi wa misaada na raia na kuendeleza ushirikiano wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran katika utekelezaji wa majukumu yake ya kibinadamu.
Katika barua hiyo, Gemma Connell, mkuu wa idara ya masuala ya kibinadamu ya shirika hilo ametoa rambirambi zake kwa familia za wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na Jumuiya kubwa ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliouawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel na kupongeza juhudi za wafanyakazi na wajitolea kwa jamuiya hiyo katika kutoa msaada kwa waathiriwa wa vita.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu pia imeashiria ripoti, nyaraka na picha zilizotolewa na mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu na kueleza wasiwasi wake kuhusu athari mbaya za vita kwa raia, hasa wanawake na watoto. Vilevile imeweka wazi uharibifu uliosababishwa na mashambulizi hayo kwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu, ofisi, magari ya misaada, magari ya wagonjwa na helikopta za Jumuiya ya Hilali Nyekundu.
Barua hiyo ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) inasisitiza kwamba kuwalinda wafanyakazi wa huduma za matibabu na wa misaada ya kibinadmu na raia wote ni miongoni mwa kanuni ya msingi ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, na inazitaka pande zote zinazohusika kuzingatia wajibu wao kwa sheria hizo.
Katika sehemu nyingine ya barua hiyo, OCHA imelaani mashambulizi yaliyosababisha mauaji au majeraha kwa raia, wakiwemo wafanyakazi wa misaada na huduma za matibabu, pamoja na uharibifu au kutia hasara vifaa na miundombinu ya misaada na raia, na kusisitiza haja ya kufika salama, haraka, na bila kizuizi wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathiriwa.