
Dar es Salaam. Mtandao wa Kitaifa wa UN Global Compact nchini Tanzania (Global Compact Network Tanzania),ameipongeza Serikali kwa moyo wake wa kuwashirikisha wadau mapema, kuiingiza sekta binafsi katika utoaji taarifa za kitaifa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), na kuoanisha ajenda ya kimataifa na malengo ya taifa kupitia Dira 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo hapa nchini,Marsha Macatta-Yambi, alipozungumza na waandishi wa habari muda mfupi ya kukamilika kwa mawasilisho hayo yaliyokuwa yakifanyika kwa njia ya mtandao jijini Newyork.
Kwa mujibu wa Marsha, hiyo ni hatua nzuri kwa kuwa sekta binafsi kupitia Global Compact Network Tanzania, imewahi kutoa taarifa zake huru za Malengo ya Maendeleo Endelevu hapo awali, mwaka 2019 na 2023.
“Katika miaka hiyo, ni baadhi tu ya mifano iliyochukuliwa kutoka kwenye taarifa hizo na kuunganishwa kwenye taarifa kuu ya VNR ya Serikali ambapo mwaka 2026, Serikali imeunganisha mifano kutoka kwenye taarifa hiyo na pia kuiambatanisha taarifa kamili ya sekta binafsi kwenye VNR yenyewe,”amesema Mkurugenzi huyo.
Akifafanua zaidi,amesema taarifa hii ilihusisha wadau zaidi ya washiriki wa UN Global Compact wakiwemo wa b iashara ndogo ,biashara za Kati (MSME) na kampuni kubwa ambapi uwe mshiriki wa mtandao au la wote waliweza kuchangia kupitia chombo kimoja kikamilifu cha utoaji taarifa.
Matokeo yake amesema sasa yameambatanishwa kwenye VNR ya kitaifa, iliyowasilishwa jana Julai 14, 2026 ambapo imejumuisha Malengo yote 17 japo malengo matano tu ndio yaliyopitiwa kimataifa kwa mwaka huu ikiwemo lengo namba 6, 7, 9, 11 na 17).
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Global Compact Network Tanzania ilibuni chombo hicho tangu mwanzo kwa mtazamo huo, kwa kuwa Malengo hayo matano hayajitengi na mengine kumi na mawili.
“Dira 2050 ni ushahidi kuwa uoanishaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Dira ulikuwa ni hatua ya makusudi, na tulwaomba wadau kuambatanisha nia hiyo na utekelezaji halisi.
Katika uwasilishaji huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa, Kitila Mkumbo, ndiye
aliyeongoza mchakato wa VNR akiwa na Tume ya Taifa ya Mipango.
Katika wasilisho hilo Waziri Kitila aliweka wazi umuhimu wake ambapi mapitio ya kimataifa ya SDG namba 6, 7, 9, 11 na 17 yanahusiana moja kwa moja na vipaumbele vya taifa. Malengo haya yanagusa msingi wa mabadiliko ya Tanzania katika maji na usafi wa mazingira, nishati safi na ya uhakika, miundombinu imara, miji endelevu, uwekaji viwanda, ubunifu, na ushirikiano imara zaidi.