
Serikali ya Sierra Leone imefuta mashtaka yake, ikiwemo ya uhaini, dhidi ya Rais wa zamani Ernest Bai Koroma, ambaye alikamatwa kuhusiana na jaribio la mapinduzi karibu miaka mitatu iliyopita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Koroma, mwenye umri wa miaka 72, amekuwa akikanusha kuhusika na jaribio la Novemba mwaka 2023 ambapo watu wenye silaha walivamia ghala la jeshi na magereza kadhaa na kuwaachilia huru karibu wafungwa elfu 2.
Akizungumza baada ya kesi dhidi yake kuondolewa, Koroma amesema mara zote amekuwa akiamini katika haki na amani na kwamba mara zote vitu hivi hushinda.
Katika taarofa yake, Koroma pia alitoa shukrani kwa rais Julius maada Bio, rais wa zamani wa Nigeria, Bola Tinubu Pamoja na jumuiya ya ECOWAS.
Punde baada ya Koroma kushtakiwa na kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani, ECOWAS iliingilia kati ambapo baadae aliruhusiwa kwenda Nigeria kwa matibabu.
Rais Koroma aliongoza nchi hiyo kwa miaka 11 hado mwaka 2018, wakati rais Bia alipochaguliwa.
Raia 11 wakiwemo wanajeshi 24 walikutwa na hatia ya kuhusika katika jaribio la mapinduzi la mwaka 2024 na kuhukumiwa vifungo tofauti jela.