Serikali ya Marekani imetangaza siku ya Jumatano kwamba itaweka ushuru wa 25% kwa bidhaa kadhaa za Brazil, kufuatia uchunguzi uliofanywa na Mwakilishi wa Biashara wa Marekani (USTR) kulingana na sheria ya mwaka 1974.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ushuru huo utaanza kutumika “mnamo Julai 22, ili kutoa muda wa utekelezaji katika mifumo ya forodha,” afisa mmoja wa Marekani amewaambia waandishi wa habari.

Washington ilianzisha uchunguzi mwaka wa 2025 kuhusu mbinu kadhaa za biashara ambapo serikali ya Marekani ililaumu Brazil, na kuifanya kuwa nchi ya kwanza kulengwa na ushuru huu mpya.

Bidhaa zilizosamehewa “ni zile ambazo hazizalishwi au kulimwa nchini Marekani, au ambazo zingekuwa na athari kwenye minyororo ya usambazaji au uchumi, kama vile machungwa, baadhi ya bidhaa  za nishati, au baadhi ya vipuri vya ndege,” afisa huyo wa Marekani ameelezea.

Uchunguzi huo, ulioanza mwaka wa 2025, ulilenga masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya ufisadi, ulinzi wa Haki miliki ya uvumbuzi, na matokeo ya ukataji miti kinyume cha sheria.

Lakini ushuru mpya pia unazingatia maamuzi ya mahakama ya Brazil kuhusu uchumi wa kidijitali, ambao Washington inauona kama “vizuizi vya biashara visivyo vya haki,” hasa zile zinazohitaji majukwaa ya mitandao ya kijamii “kuondoa baadhi ya maudhui ya kisiasa” au kuweka “adhabu kwa kutofuata sheria.”

Ofisi ya rais wa Brazil ilifutilia mbali uamuzi wa Marekani usiku wa Jumatano kuamkia siku ya Alhamisi, ukiona “hakuna uhalali” wake. “Hakuna uhalali wa hatua za upande mmoja dhidi ya nchi yetu,” ilisema ofisi ya Rais Luiz Inácio Lula da Silva katika taarifa kwa vyombo vya habari. Ofisi ya rais unapinga  “madai” yote yaliyotolewa na Washington kuhusu “mazoea ya biashara yasiyo ya haki yanayodhaniwa kupitishwa na Brazil.”

Mwishoni mwa mwezi wa Februari, Mahakama Kuu ya Marekani ilifuta sehemu kubwa ya ushuru uliotafutwa na rais wa Marekani, ikiamua kwamba alikuwa ametafsiri vibaya sheria ili kuhalalisha. Ushuru maalum wa sekta, unaolenga viwanda kama vile magari, chuma, alumini, na shaba.

Suala la kisiasa nchini Brazil

Washington kwa upana zaidi inaishutumu Brasília kwa kutumia ushuru wa upendeleo kwa bidhaa za Mexico na India kwa uharibifu wa bidhaa za Marekani, hali ambayo ni “hasara ambayo haiendani na majukumu ya kimataifa”.”

Ushuru uliowekwa na Marekani umekuwa suala la kisiasa nchini Brazil, ambapo uchaguzi wa rais, umepangwa kufanyika mwezi Oktoba, unakaribia.

Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva alimkosoa mpinzani wake Flávio Bolsonaro, mtoto wa Rais wa zamani Jair Bolsonaro, mwanzoni mwa mwezi kwa kuiomba Marekani “kuahirisha” utekelezaji unaowezekana wa ushuru mpya wa Marekani hadi baada ya uchaguzi.

Na mwanzoni mwa mwezi Julai, Rais wa kihafidhina Flávio Bolsonaro alisafiri hadi Washington kushiriki katika kikao cha hadhara cha USTR kuhusu suala hilo, akitumia fursa hiyo kudai kwamba ushuru mpya ungemnufaisha rais aliye madarakani wa mrengo wa kushoto, ambaye alikuwa akigombea kuchaguliwa tena.

Rais wa Marekani Donald Trump ameufanya ushuru kuwa moja ya silaha zake kuu za kiuchumi, akiweka mfululizo wa ushuru mpya kwa bidhaa zote zinazoingia nchini Marekani.

Alikuwa ameilenga Brazil haswa, akiweka ushuru wa hadi 50% kwa bidhaa kadhaa kulipiza kisasi kwa hatia, ambayo aliiona kuwa ya kisiasa, ya Jair Bolsonaro, aliyepatikana na hatia ya kushiriki jaribio la mapinduzi.

Kutokana na athari ya mfumuko wa bei ya ushuru mpya, Washington ilikuwa imefuta ushuru ulilenga bidhaa kadhaa za kilimo, ikiwa ni pamoja na nyama ya ng’ombe, kahawa, na nyanya za Brazil.

Kulingana na data ya USTR, Marekani ilisafirisha bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 54 kwenda Brazili mwaka wa 2025, na kuagiza karibu dola bilioni 40 kwa wakati mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *