Mkuu wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) ameapa kwamba Jamhuri ya Kiislamu itaendeleza mashambulizi yake ya kulipiza kisasi “yenye ufanisi” hadi utulivu utakaporejeshwa kote nchini.

“Ufyatuaji wetu wa makombora wenye ufanisi na uliolenga shabaha kwa usahihi kutoka kote nchini Iran dhidi ya adui utaendelea hadi utulivu utakaporejea katika pwani ya kusini na Lango-Bahari la Hormuz,” amesema Brigedia Jenerali Sayyid Majid Mousavi katika ujumbe uliotolewa jana Ijumaa.

Amesisitiza kwamba hakuna tofauti kati ya mji mkuu na kusini mwa nchi na kwamba mashambulizi yoyote dhidi ya maeneo hayo yatashughulikiwa kwa usawa.

“Mtazamo wetu ni kwamba ardhi ni ardhi; Tehran na maeneo ya kusini mwa nchi vinaunda ardhi moja ya Iran,” amesisitiza kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC.

Katika siku chache zilizopita, jeshi la kigaidi la Marekani limefanya mashambulizi makali Kusini mwa Iran na kurejesha mzingiro wa bandari za Iran, jambo ambalo ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya kukomesha vita.

Vikosi vya jeshi la Iran vimefanya mashambulizi makali ya kulipiza kisasi dhidi ya kambi za kijeshi na maeneo ya kimkakati ya Marekani katika eneo lote la Magharibi mwa Asia, na kutangaza kwamba njia ya maji ya kimkakati ya Lango Bahari la Hormuz imefungwa “hadi taarifa nyingine itakapotolewa.”

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pia limeshambulia kituo cha amri ya operesheni maalumu za Marekani nchini Syria, maeneo ya rada ya jeshi la utawala huo huko Oman, na maghala ya silaha na vituo vya kufyatulia makombora nchini Kuwait.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa jioni, Idara ya Mahusiano ya Umma ya IRGC ilisema kwamba katika operesheni iliyofanywa na Jeshi la Anga, mfumo wa rada na helikopta kadhaa za operesheni maalumu za Marekani zimeharibiwa huku idadi kubwa ya wanajeshi wahalifu wa Marekani wakiuawa.

Ni vyema kuashiria hapa kuwa Marekani na vyombo vya habari vya Magharibi na washirika wao wa Kiarabu vimekuwa na tabia ya kuficha hasara na idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaouawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Jamhuri ya Kiislamu.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *