Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance aliishambulia Israel na kuishutumu kuwa inajaribu kushawishi siasa za Marekani, akisisitiza kuwa umaarufu wake umepungua nchini Marekani.

Pia amefichua uhusiano uliokuwepo kati ya bilionea mhalifu wa ngono aliyehukumiwa na kufia gerezani, Jeffrey Epstein, na idara ya ujasusi ya Israel, Mossad.

Wakati wa mahojiano ya masaa matatu kwenye podikasti maarufu ya Marekani, J.D Vance ameituhumu Israel kuwa inajaribu kuvuruga mazungumzo kati ya Washington na Tehran, akiashiria majaribio ya baadhi ya viongozi wa serikali ya Israel ya kutaka kuathiri sera ya Marekani, hasa kupinga na kuzuia makubaliano na mazungumzo yanayofanywa baina ya utawala wa Marekani na Iran.

Vance pia ametoa ushahidi kwa kuashiria ripoti iliyochapishwa katika jarida la Time ikifichua kampeni ya ushawishi wa siri iliyofadhiliwa na Israel, iliyolenga moja kwa moja kuvuruga mazungumzo na kuzuia makubaliano baina ya Washiington na Tehran.

Makamu wa Rais wa Marekani amesema kwamba ripoti hiyo imefafanua kwamba vyombo ndani ya serikali ya Israel vilimlipa pesa mtu ambaye hapo awali alifanya kazi katika kampeni ya Trump, ambaye naye alisambaza pesa hizo kwa watu wenye ushawishi ndani ya Marekani ili kushambulia makubaliano hayo, kumshambulia Vance binafsi, na kumchafulia jina.

Vance amedai kwamba anajua “bila shaka yoyote” kwamba kuna watu katika serikali ya Israel wanaodanganya maoni ya umma ya Marekani na kujaribu kuelekeza sera ya Marekani upande wa kuendeleza vita dhidi ya Iran kwa muda usiojulikana, badala ya kufikia suluhu au suluhisho la kidiplomasia ambalo lingekomesha mapigano.

Vance amesema kwamba Israel “kwa sasa inapoteza vita vya maoni ya umma nchini Marekani,” jambo ambalo amesema ni uhakika unaoonekana dhahiri, hasa kwa kutilia maanani pengo la maoni kati ya vijana na Warepublican walio na umri wa zaidi ya miaka 65.

Katika mahojiano hayo J.D Vance amethibitisha kwamba mhalifu mashuhuri wa ukatili wa ngono dhidi ya watoto, Jeffrey Epstein, alikuwa na uhusiano na viongozi wa ngazi za juu zaidi wa taasisi za ujasusi za Israel na Marekani.

Makamu wa rais wa Marekani amesema Ikulu ya White House “ilishughulikia vibaya” mafaili ya Epstein, akidai kwamba serikali ya Marekani ilipaswa kuyafichua mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *