.

Chanzo cha picha, Getty Images

Jeshi la Marekani limesema limefanya mashambulizi kwa
usiku wa saba mfululizo dhidi ya Iran tangu Rais Donald Trump atangaze
makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda “yamefutiliwa mbali”.

Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa X, Kamandi
Kuu ya Marekani (Centcom) iliandika kwamba vikosi vyake “vimeshambulia
maeneo ya uchunguzi, miundombinu ya vifaa vya kijeshi, maghala ya silaha yaliyopo chini ya
ardhi, na uwezo wa
kijeshi wa majini”.

Jeshi la
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) lilisema meli mbili za mafuta
zililipuka katika Mlango-Bahari wa Hormuz wakati zikipita kwenye sehemu ya njia ya meli
iliyokuwa na mabomu ya ardhini. Taarifa hiyo ilipuuzwa na Hata hivyo, Centcom ilisema
kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Vikosi vya
kijeshi vya Jordan vilisema vilidungua makombora 10 ya Iran yaliyorushwa kwenye
anga yake usiku huo, ingawa hakukuwa na majeruhi wala uharibifu wowote.

Centcom
ilisema kuwa ilimaliza mashambulizi yake saa 21:30 kwa saa za Marekani
Mashariki (02:30 BST) baada ya kufanya mashambulizi hayo kwa muda wa saa
kadhaa.

Katika
taarifa yake, Centcom ilisema: “Vikosi vya Marekani vilitumia ndege za
kivita, ndege zisizo na rubani, na meli za kivita pamoja na vifaa vingine
katika operesheni hiyo.”

Shirika la
habari la serikali ya Iran, Fars, lilisema meli mbili za mafuta “zililipuka na kushika moto wakati zikipita kwenye njia iliyokuwa na
mabomu ya ardhini kusini mwa Mlango wa Hormuz”. Baadaye, Centcom iliandika
kwenye X: “Kama madai mengi ya IRGC, hii si kweli.”

Usafirishaji
wa meli katika Mlango muhimu wa Hormuz umesitishwa kwa kiasi kikubwa kutokana
na kuendelea kwa mashambulizi ya kulipizana kisasi kati ya vikosi vya Marekani
na Iran.

Soma Zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *