Katika taarifa hiyo, viongozi hao wameleza kuwa msaada huo wa dharura unahitajika kwa haraka ili kukidhi mahitaji ya msingi ya mamilioni ya watu walioathirika na mzozo unaoendelea nchini Sudan, ambao umechochea moja ya migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani kwa sasa.

Zaidi ya watu milioni 12  wamekimbia makazi Yao

Nilibebwa kwenye mabega ya watoto wangu kwa siku 40 nikiwa kwenye kiti hiki cha magurudumu, “anasema Al-Sayed, mwenye umri wa miaka 70, ambaye alilazimika kukimbia kutokana na machafuko ya kivita katika Jimbo la Aj Jazirah mnamo mwezi Oktoba 2024. “Watu walikuja kwa miguu, wengine walitembea kwa siku tatu, wengine kwa wiki nzima na wengine kwa siku 10. Wengine walifariki njiani kwa kiu, mateso, na uchovu,” amesisitiza.

Inakadiriwa kuwa watu milioni 12.4 wamekimbia makazi yao kote nchini Sudan tangu mwezi Aprili 2023, karibu milioni 9 wakiwa wakimbizi wa ndani, huku zaidi ya milioni 3.3 wakikimbilia nchi jirani. Safari yao ya kutafuta hifadhi imejaa hatari na mateso makubwa.

Katika eneo la Gedaref, takribani saa 6 kutoka Khartoum karibu na mpaka wa Eritrea, kituo cha zamani cha mabasi kimegeuzwa kuwa kambi ya wakimbizi wa ndani. Kituo hiki kina wakazi wapatao 6,600 waliowasili wakati wa wimbi la tatu la watu kukimbia kutoka maeneo ya Sinjar/Sannar kusini mwa Khartoum mnamo mwezi Julai 2024.

Mateso hayaishii njiani tu  yanazidi baada ya kuwasili, ambako kuna mbu wanaoeneza magonjwa na usiku wenye baridi kali ambao hutishia maisha.

Wagonjwa wanapokea matibabu katika chumba cha hema nje ya hospitali huko Khartoum, kwani mfumo wa afya wa Sudan unakabiliwa na mkazo mkubwa kutokana na mashambulizi, uhaba, milipuko ya magonjwa na majanga ya asili.

© UNICEF/Ahmed Mohamdeen Elfatih

Wagonjwa wanapokea matibabu katika chumba cha hema nje ya hospitali huko Khartoum, kwani mfumo wa afya wa Sudan unakabiliwa na mkazo mkubwa kutokana na mashambulizi, uhaba, milipuko ya magonjwa na majanga ya asili.

Watu wanakufa

Kifo kinawazunguka watu kila kona ya Sudan. Mizinga na mashambulizi ya anga yanaendelea bila kukoma, yakiua na kujeruhi raia, huku mashambulizi dhidi ya wahudumu wa afya na vituo vya afya yakisababisha madhara makubwa. Mfano wake ni shambulio la ndege isiyo na rubani lililotokea  tarehe 24 Januari kwenye hospitali ya Saudi Teaching Maternal  Hospital huko Al Fasher  hospitali ya mwisho yenye uwezo wa kufanya upasuaji katika eneo hilo ambalo limesemekana kuua takribani watu 70 na kuwajeruhi wengine wengi.

Njaa imethibitishwa katika maeneo matano

Njaa imefikia viwango vya kihistoria, huku watu karibu milioni 25 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Kwa wakati huo huo, milipuko ya magonjwa na athari za mabadiliko ya tabianchi zimezidisha hali ya dharura.

Njaa ni hali ambayo angalau mtu moja kati ya kaya tano hukumbwa na uhaba wa chakula uliokithiri, hali inayoweza kupelekea utapiamlo mkali na vifo. 

Njaa imethibitishwa katika Milima ya Nuba Mashariki na Darfur Kaskazini, na hali kama hiyo inatarajiwa kuenea katika maeneo mengine matano hadi kufikia mwezi Mei 2025.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), linakadiria kuwa watoto wapatao 770,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wamekumbwa na utapiamlo mkali  na hatari zaidi kuliko mwaka  wa 2025. Watoto wenye hali hii wako katika hatari mara kumi zaidi ya kufariki dunia kutokana na maradhi, ikilinganishwa na watoto wenye afya njema.

Takriban watu milioni 6.7 wako katika hatari ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia nchini Sudan, huku wanawake na wasichana waliokimbia makazi yao, wakimbizi na wahamiaji wakiwa hatarini zaidi.

© UNICEF/Mohamed Zakaria

Takriban watu milioni 6.7 wako katika hatari ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia nchini Sudan, huku wanawake na wasichana waliokimbia makazi yao, wakimbizi na wahamiaji wakiwa hatarini zaidi.

Kuzuka kwa unyanyasaji wa kijinsia

Ukandamizaji wa kijinsia umeongezeka kwa kiwango cha kutisha. Zaidi ya wanawake na wasichana milioni 12.2, pamoja na ongezeko la waathirika wanaume na wavulana, wako katika hatari ya ukatili wa kijinsia kote Sudan, idadi hii ni ongezeko la asilimia 80 ikilinganishwa na mwaka uliopita. 

Wanawake na wasichana kwa kiwango kikubwa wanaendelea kukumbwa na manyanyaso, ikiwa ni pamoja na ubakaji unaohusiana na vita.

Magonjwa yanaenea

Chini ya robo moja ya vituo vya afya vinafanya kazi katika maeneo yaliyoathirika zaidi. Magonjwa kama kipindupindu, homa ya dengue, na malaria yanaenea kwa kasi.

Mnamo mwezi Agosti 2024, kambi ya wakimbizi wa ndani ya Minaa El Bar iliyokuwa kituo cha mabasi hapo awali  ilikumbwa na mlipuko mkubwa wa kipindupindu uliowaathiri zaidi ya watu 2,000 waliokuwa wamekimbia mashambulizi kutoka Khartoum na Aj Jazirah.

Mfumo wa afya ulioporomoka umewaathiri pakubwa watu wenye maradhi ya muda mrefu. Mohamed Abdullah Mohamed, mwenye umri wa miaka 40, alikuwa mwalimu wa watu wenye ulemavu wa kuona huko Khartoum. Sasa, baada ya kupoteza kazi na kuwa tegemezi kabisa kwa misaada ya kibinadamu, Mohamed anahangaika kupata huduma za matibabu kwa tatizo lake la macho.

Mke wangu pia ni kipofu, hivyo sina mtu wa kushirikiana naye kulea watoto wetu watano,” amesema.

Takriban watu milioni 18 kote nchini Sudan wanakabiliwa na njaa kali.

Nearly 18 million people across Sudan are facing acute hunger.

Takriban watu milioni 18 kote nchini Sudan wanakabiliwa na njaa kali.

Watoto milioni 17 hawako shuleni

Ningependa nirudi shule. Kwangu mimi na watoto wengine katika kambi hii ya wakimbizi wa ndani, elimu imesimama kabisa tangu mzozo ulipoanza,” amesema Ibrahim, mwenye umri wa miaka 18, aliyekuwa darasa la nane kabla ya mgogoro.

Mamilioni ya watoto wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan, wakikumbwa na miezi ya sintofahamu, kiwewe na ukatili. 

Zaidi yao, milioni 17 hawapo shuleni kote nchini Sudan, huku zaidi ya milioni moja wakiwa kwenye hali ya sintofahamu kutokana na kutofanyika kwa mitihani ya kitaifa ya sekondari tangu mwaka 2023. Mamia ya shule kote nchini zinatumika kama makazi ya wakimbizi, hali inayozidi kuvuruga mfumo wa elimu.

UNICEF  imesema hali ya sasa nchini Sudan ni  janga la Watoto  linalozidi kuongezeka, likitishia kwa kiwango kikubwa mustakabali wa nchi hiyo na kuathiri kwa undani kanda nzima.

Mwitikio wa kibinadamu wakabiliwa na changamoto kubwa

Licha ya misaada ya kibinadamu kuwafikia watu katika maeneo mengi, vizuizi vya upatikanaji  hasa kwenye maeneo yenye mapigano makali  na uhaba wa fedha vinaendelea kuzuia utoaji wa misaada pale inapohitajika zaidi.

Misaada kutoka Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) na Mfuko wa Kibinadamu wa Sudan (SHF) imehakikisha utoaji wa msaada muhimu kwa watu walio hatarini zaidi kutokana na mzozo, ikiwa ni pamoja na huduma za afya (ikiwemo huduma za afya ya uzazi), lishe, makazi, maji na huduma za ulinzi. Angalau watu milioni 4.7 wamepata msaada kupitia CERF, na milioni  7.7  kupitia shughuli zilizoungwa mkono na SHF.

Hata hivyo, mahitaji bado ni makubwa. Mpango wa Mahitaji ya Kibinadamu na Mwitikio wa Sudan kwa mwaka huu unahitaji rekodi ya dola bilioni 4.2 , huku UN na washirika wake wakilenga kuwafikia watu  milioni 20.9  kwa msaada wa haraka wa kuokoa maisha. Miongoni mwao, watu milioni  3.2  wanapata huduma zinazohusiana na ukatili wa kijinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *