
Kampuni ya Ufaransa ya TotalEnergies imethibitisha siku ya Jumamosi, Oktoba 25, kuanza tena kwa mradi wake mkubwa wa gesi katika eneo la Cabo Delgado nchini Msumbiji. Licha ya tishio la wanajihadi linaloendelea kaskazini mwa nchi, rais wa nchi hiyo anafanya kazi ya kuanzisha upya miradi ya maendeleo ya gesi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maputo pia hivi karibuni ilisaini makubaliano na kampuni ya ENI ya Italia, na rais wa Msumbiji anatarajiwa katika makao makuu ya kampuni nyingine kubwa, Exxon Mobil, nchini Marekani, kuendeleza mradi wa tatu.
Mkurugenzi Mtendaji wake, Patrick Pouyanné, alitangaza hilo mwishoni mwa mwezi Juni, na sasa ni rasmi: Total Energies imethibitisha siku ya Jumamosi, Oktoba 25, 2025, kwa shirika la Agence France Presse (AFP) kuanzisha tena mradi wake mkubwa wa-gesi huko Cabo Delgado, Msumbiji.
kampuni ya msumbiji ya LNG, inayoongozwa na kampuni ya Ufaransa, imeondoa udharura” uliotangazwa kufuatia shambulio kubwa la wanajihadi katika jiji la Palma, ambalo liliwaua zaidi ya watu 800 mwaka wa 2021 na kusababisha kusimamishwa kwa shughuli.
Mradi wa gesi asilia iliyoyeyushwa unawakilisha uwekezaji wa dola bilioni 20, huku shughuli zikitarajiwa kuanza mwaka wa 2029. TotalEnergies sasa inasubiri idhini kutoka kwa mamlaka ya Msumbiji. Hili halipaswi kuchukua muda mrefu, kwani Rais Daniel Chapo mwenyewe aliomba kuanza tena kwa shughuli za kampuni hiyo ya Ufaransa.
Rais anataka kufufua miradi ya maendeleo ya gesi
Kiongozi wa Nchi analenga kufufua kwa kina sekta ya gesi. Mapema mwezi huu, alisaini makubaliano na kampuni kubwa ya mafuta na gesi ya Italia ENI kwa ajili ya uendeshaji wa jukwaa jipya la pwani, Coral Sul, ifikapo mwaka wa 2028, ambalo lingeongeza uzalishaji wa sasa wa LNG mara mbili.
Siku ya Jumamosi, Rais wa Msumbiji alisafiri hadi Marekani, ambapo amepangwa kutembelea makao makuu ya Exxon Mobil. Kampuni hiyo ya Marekani, ambayo ni kampuni kubwa ya hidrokaboni, imekuwa kijihusisha na mradi mwingine mkubwa, Rovuma LNG, ikisema ilikuwa inasubiri uamuzi wa TotalEnergies kabla ya kujitolea zaidi kwa Msumbiji.
Miradi hii yote imekosolewa vikali na wanaharakati wa mazingira na inaambatana na shutuma za ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na jeshi la Msumbiji.