Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Yao Agbetse, amewasilisha ripoti yake ya kila mwaka kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, Oktoba 29. Licha ya kuboreka kwa hali wa jumla katika miaka ya hivi karibuni, hali bado inatia wasiwasi kaskazini-mashariki na kusini-mashariki mwa nchi, hasa wakati ukikaribia Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 28.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makundi yenye silaha yanasalia kuwa wahusika wakuu wa ukosefu wa usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Unyanyasaji na ukatili wao unaendelea, licha ya ahadi zilizotolewa katika makubaliano ya amani ya hivi karibuni. Lakini vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) pia vinanyooshewa kidole kwa  kukamata watu kiholela, kuwaweka kizuizini, na mauaji ya watu walio mikononi mwa vyombo vya dola, na kushindwa kuwalinda raia kutokana na ukosefu wa vifaa unaoendelea.

Pia kunaripotiwa unyang’anyi na vurugu, vitendo ambavyo vinahusishwa washirika wao wa Urusi, ambapo wameshindwa kufanya uchunguzi unaofaa, ripoti inasema, kuzuia unyanyasaji unaofanywa na kundi la Azande walilolifunza kusini-mashariki kupambana na waasi wa UPC.

“Ninatoa wito kwa mamlaka kushiriki katika mazungumzo” Wanamgambo wanashutumiwa kwa mauaji, ubakaji wa  watu wengi, na mateso, hasa wakiwalenga Wafulani na Waislamu, na hivyo kufufua mvutano kati ya jamii. “Ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kusimamisha shughuli za Azande, inaonekana kwangu kwamba tuko katika matatizo makubwa katika suala la usalama,” anasema Yao Agbetse, mtaalamu huru kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Hili ni tishio linaloendelea, miezi miwili kabla ya uchaguzi wa urais, ambapo watu kadhaa wa upinzani, kama vile Anicet Georges Dologuélé, wanaweza kuenguliwa.

“Ninatoa wito kwa mamlaka kushiriki katika mazungumzo na kuhakikisha kwamba mazungumzo haya yanatoa majibu muhimu ili baadhi ya viongozi wa upinzani wasiondolewe katika mchakato wa uchaguzi, ikizingatiwa kwamba ninaona uchaguzi huu kuwa hatua muhimu kwa nchi,” Yao Agbetse ameongeza.

Baraza la Katiba linakamilisha mapitio yake ya wagombea leo Alhamisi, Oktoba 30, na linatarajiwa kutoa katika siku zijazo orodha ya wagombea watakaoidhinishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *