
Mtandao wa madaktari nchini Sudan umeishtumu kundi la wapiganaji wa RSF, kwa kujaribu kuficha ushahidi wa mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur kwa kuchoma miili au kuzika miili ya watu waliouawa katika makaburi ya pamoja.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mtandao wa madaktari wa Sudan, umesema siku ya Jumapili kwamba wapiganajai hao wamekuwa wakikusanya mamia ya miili kwenye barabara za mji wa El- fasher jimboni Darfur Magharibi, tangu wadhibiti mji huo Oktoba 26.
Madaktari hao wametaja kuzikwa kwa miili ya raia waliouawa kama mauaji ya kimbari na ukiukaji wa kanuni zote za kimataifa na kidini zinazokapinga kukatwa viungo vya miili na kuwahakikishia waliofariki haki ya kupewa mazishi ya heshima.
Aidha mtandao huo umesema kuwa uhalifu uliofanywa na RSF hauwezi kufutwa kwakuchoma au kuzika miili, na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka katika kuanzisha uchugnguzi huru wa kimataifa kuhusiana na ukatili dhidi ya raia katika mji wa Al Fasher.
Mnamo Oktoba 26, RSF ilitwaa mji wa El- Fasher, mji mkuu wa Darfu Kaskazini, na kutekeleza mauaji ya halaiki, kwa mujibu wa ripoti za mashirika ya ndani na kimataifa.
Vita nchini Sudan vilivyoanza Aprili 2023, kati ya jeshi na RSF, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, huku mamilioni ya watu wakisalia wakimbizi wa ndani na nje ya taifa hilo.