Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR, majanga ya mabadiliko ya tabianchi tayari yameshawalazimisha mamilioni ya watu ulimwenguni kuwa wakimbizi.

UNHCR imesema hayo kuelekea mkutano wa kila mwaka wa tabia nchi COP 30 unaoanza Jumatatu nchini Brazil.

Kulingana na ripoti ya UNHCR iliyotolewa Jumatatu, katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, majanga yanayohusiana na hali ya hewa, yamesababisha takriban watu milioni 250 kuhama ndani ya nchi zao, hiyo ikiwa sawa na zaidi ya watu 67,000 kila siku.

UNHCR imetaja majanga kama mafuriko nchini Sudan Kusini na Brazil, viwango vya juu vya joto vilivyoshuhudiwa Kenya na Pakistan pamoja na uhaba wa maji nchini Chad na Ethiopia.

Ripoti ya UNHCR ilibainisha kwamba mabadiliko ya tabianchi “yanaongeza na yanaimarisha changamoto zinazowakabili wale ambao tayari wameshakuwa wakimbizi, na pia wenyeji wao, hasa kwenye mazingira tete na yenye migogoro mingine.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *