Wabunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanatarajiwa kupiga kura kumchagua spika mpya, miezi miwili kadhaa baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika Vital Kamerhe.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa zamani wa viwanda Aimé Boji, anayeungwa mkono na muungano wa Sacred Union wake rais Felix Tshisekedi, anatarajiwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo.

Kuelekea uchaguzi huo, chama cha UNC kinachoongozwa na Kamerhe, hakikuwasilisha mgombea kwenye nafasi hiyo, yenye ushawishi kwenye siasa DRC.

Iwapo atachaguliwa Spika, Boji, atakuwa mwanasiasa mwingine mashuhuri kushika wadhifa huo mkubwa kutoka jimboni Kivu Kusini, Mashariki mwa nchi hiyo kama alivyokuwa Kamerhe.

Wachambuzi wa siasa wanasema, huu ni mpango wa rais Tshisekedi, kuendelea kuhakikisha kuwa anaendelea kushawishi eneo la Mashariki kisiasa.

Hata hivyo, jina la Aimé Boji linapingwa na wanasiasa wa upinzani, walio ndani na nje ya nchi, wakati wabunge wanapojiandaa kupiga kura siku ya Alhamisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *