
Takriban wapiga kura milioni 6.7 wameitwa kwenye uchaguzi mnamo Desemba 28 nchini Jamhuri ya Guinea, kati ya idadi ya watu inayokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 14.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uchaguzi huu wa rais utaashiria kurejea kwa utaratibu wa kikatiba, ambao ulivurugwa na mapinduzi ya kijeshi mnamo Septemba 5, 2021, ambayo yalimleta Jenerali Mamadi Doumbouya madarakani.
Wagombea tisa waidhinishwa kuwania kwenye nafasi ya urais
Mahakama ya juu zaidi nchini imeidhinisha wagombea tisa, ikiwa ni pamoja na ile ya rais aliyepo, Jenerali Mamadi Doumbouya. Wote walikuwa tayari kwenye orodha ya muda iliyotangazwa wiki iliyopita na mahakama kuu hiyo. Wagombea tisa, wakiwemo wagombea binafsi wawili walioibuka washindi wiki iliyopita, wameendelea kushikilia nafasi zao. Ousmane Kaba na Lansana Kouyaté orodha zao zimekataliwa. Kuhusu Aboubacar Diakité, anayejulikana pia kama Toumba, ambaye bado anazuiliwa katika gereza la kiraia la Conakry, hakuweza kutoa hati zote muhimu.
Uchaguzi wa urais nchini Guinea utafanyika Desemba 28, 2025 kwa ajili ya kumchagua rais wa jamhuri kati ya wagombea tisa walioidhinishwa na Mahakama Kuu.