Mwigulu anakuwa Waziri Mkuu wa 12 wa Tanzania tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake.
Spika Mussa Zungu alipokea hati ya uteuzi huo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kutangaza mbele ya wabunge kwa ajili ya kumthibitisha kwa kura kwa mujibu wa ibara ya 51 kifungu kidogo cha cha pili cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya hatua hiyo wabunge walipiga kura na kumuidhinisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Tanzania, matokeo yaliyosomwa bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Hamza Johari.
“Muheshimiwa daktari Mwigulu Nchemba amethibitishwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu kwa jumla ya kura mia tatu sitini na tisa.”
Akizungumza mara baada kuteuliwa na kupigiwa kura kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu, amesema kuwa anatambua bado Watanzania wengi wanakabiliwa na lindi la umasikini na pia nchi hii ni ya Watanzania wote na watasikilizwa kwa nidhamu katika ofisi za umma na akawanyoshea kidole watumishi wa umma walio wavivu, wazembe na wala rushwa.
“Kwa watumishi wa umma, wavivu, wazembe na wala rushwa tuwe tayari” alisema huku akishangiliwa na wabunge.
Aliongeza kuwa hatakuwa na simile kwa watumishi wa umma ambao hawatakwenda na kasi ya serikali katika kuleta maendeleo kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.
Wachambuzi: Mwigulu ni chaguo sahihi
Kuteuliwa kwa Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, kumewaibua wachambuzi wa masuala ya siasa nchini humu, akiwemo Marcel Hamduni ambaye anasema kuwa Mwigulu ni mchapakazi, lakini anayo kazi kubwa kuuthibitishia umma kama anaweza kuwa mwadilifu.
“Kazi aliyonayo mbele yake ni kubwa sana na anahitaji kuuthibitishia umma kwamba anaweza kuwa muadilifu.”
Nao wananchi wa kawaida wamekuwa na maoni mseto kuhusu uteuzi huo. Ikiwemo wale ambao wanakubaliana na uchaguzi huKanisa Katoliki Tanzania: Kuua waandamanaji ni aibu kwa nchiu na wale ambao wanapinga wakisema wanayo mashaka namna ambavyo atachangia katika kuleta ustawi wa kiuchumi.
Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanasema rekodi yake katika masuala ya kifedha inaridhisha.
Kitaaluma Mwigulu Nchemba ni mchumi, kada wa muda mrefu wa chama tawala cha CCM akimrithi Kassim Majaliwa anayemaliza muda wake.
Mwanasiasa huyo wa muda mrefu, alikuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
