Wabunge nchini Jamuhruri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemchagua Waziri wa zamani Aimé Boji, kutoka muungano wa kisiasa  wa Sacred Union wake rais Felix Tshisekedi, kuwa Spika mpya.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Aimé Boji, Waziri wa zamani wa bageti na viwanda  aliyependekezwa kama mgombea pekee kutoka muungano wa Union Sacrée wake rais Felix Tshisekedi, anakuchaguliwa kwenye wadhifa huo. 

Upinzani ambao unastahili kuchukua nafasi ya Naibu muwazilishaji wa taarifa za bunge, hawakuwa na makubaliano, Mutita Kalunga Clotilde toka chama cha Ensemble Pour la République ya Moïse Katumbi, alichaguliwa kwenye nafasi hio lakini Christelle Vuanga, mwana chama wazamani wa Ensemble, amesema, chama hicho kilitumia njama ili kuondoa ugombea wake. 

Kuelekea uchaguzi huo, chama cha UNC ya Kamerhe, hakikuwasilisha mgombea kwenye nafasi hiyo, yenye ushawishi kwenye siasa DRC.

Hata hivyo, jina la Aimé Boji linapingwa na wanasiasa wa upinzani, walio ndani na nje ya nchi, waki mushtumu kuwa karibu na Raïs Tshisekedi na abaeye anaweza kumupa fursa ya kusalia madarakani kwa kudirisha katiba. 

Freddy Tendilonge/ Kinshasa/ RFI Kiswahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *