Jeshi nchini  Sudan limesema vikosi vyake siku ya Alhamisi  vimeanzisha mashambulio kwa kutumia  ndege zisizo na rubani kulenga mji wa kaskazini wa Merowe, ulio na bwawa kubwa, katika jimbo la Kordofan wakati huu vita vikiendelea kushuhudiwa kati yao na vikosi vya wanamgambowa RSF.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo yanajiri wakati huu dunia ikiendelea kushuhudia hali mbaya ya kibinadamu inayosababishwa na mapigano yasiyokoma, yanayoendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo tangu Aprili 2023.

Ghasia zimeongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni, huku RSF ikichukuwa udhibiti wa mji muhimu wa El-Fasher na kushtumiwa kutekeleza mauaji ya maelfu ya raia wasiokuwa na hatia.

Taarifa za jeshi la sudan zinasema Siku ya Alhamisi, ndege zisizo na rubani “zililenga makao makuu ya jeshi, uwanja wa ndege na Bwawa la Merowe” huku baadhi ya ndege hizo zikinaswa  

Vita kati ya jeshi na vikosi vya RSF vimeua makumi ya maelfu ya watu, na kuwafanya wengine karibia milioni 12 kuyahama makazi yao na kusababisha moja ya migogoro mbaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *